SHEIKHE ALI AMMAR MWAZOA: "BARUA YA KIONGOZI MUADHAMU IMETOKA WAKATI AMBAO ULIMWENGU WA MAGHARIBI UNAFANYA KILA HILA.

Sheikh Ali Ammar Mwazoa mwanaharakati mashuhuri wa Kiislamu wa Tanga, Tanzania amesema kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwa vijana wa nchi za Magharibi ina thamani kubwa na imetolewa wakati mwafaka.
Sheikh Ali Ammar amesema kuwa, barua hiyo ya Kiongozi Muadhamu imetolewa katika wakati ambao ulimwengu wa Magharibi unafanya kila hila kuwahadaa w
alimwengu kuhusiana na matukio mbalimbali ulimwenguni.

Mwanaharakati huyo na mchambuzi wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu amesema, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu inawaamsha vijana wa Magharibi na kuwataka wafahamu vyema mambo yanayojiri hivi sasa ulimwenguni na kutohadaika na propaganda chafu.

Sheikh Ali Ammar Mwazoa amekosoa propaganda za madola ya Magharibi na kulaani undumakuwili wa madola hayo kuhusiana na masuala mbalimbali likiwemo suala la haki za binadamu. Amesema, madola ya Magharibi yamekuwa yakifanya propaganda ili kuwafanya walimwengu wakubaliane na misimamo yao.

Sambamba na kuelezea umuhimu wa barua ya Kiongozi Muadhamu kwa vijana wa Magharibi, Sheikh Ali Ammar amesema kuwa madola ya Magharibi yamepoteza mwelekeo kwani yamekuwa yakitanguliza mbele maslahi yao hata kama hilo litatimia kwa gharama ya roho za watu na kuvunja heshima za watu na utu wao.

Kadhalika mwanaharakati huyo wa Kiislamu wa Tanga, Tanzania ameyakosoa baadhi ya madola ya Kiarabu yanayotumiwa na Wamagharibi kwa ajili ya kusukuma mbele malengo ya maadui wa Uislamu. Chanzo cha habari: 
http://kiswahili.irib.ir/barua-ya-kiongozi/item/53545-