KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W)


Waumini wa dini ya Kiislamu Mkoani Tanga wameungana na Waislamu wenzao duniani katika kukumbuka siku ya kifo cha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w). 

Tarehe 28 mwezi Swafar mwaka 11 A.H. ilikuwa ni siku ya huzuni sana kwa wapenzi wa kiumbe bora aliyewahi kutembea katika mgongo wa ardhi, ambaye siyo rais wa nchi fulani, na wala siyo katibu wa Umoja wa Mataifa (UN), bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, mtume wa kwanza kabisa kuumbwa katika ulimwengu wa nuru na vitu vyote vikategemea nuru yake, na wa mwisho kabisa kutumwa katika mgongo wa Ardhi, Mtume Muhammad S.A.W.W. ambaye ndiye aliyekuja na ustaarabu huu ambao tunaushuhudia leo katika ulimwengu wakiislam; tunu za amani, huruma, elimu, upendo, na utamaduni. Hivi vilikuwa ni vipaumbele vya kiongozi huyu adhimu.
Kwa huzuni kubwa, suala la kifo cha mtume Muhammad S.A.W.W. limekuwa ni kitendawili kinachokosa mteguaji kwa watu wengi katika jamii zetu zinaotuzunguka. Ukimuuliza mtoto mdogo wa Madrasa zetu za mtaani kuhusu tarehe aliyozaliwa Mtume S.A.W.W. atakwambia tena kwa haraka sana pasina kufikiria.

Lazima tutafakari zaidi nini tatizo mpaka siku hii ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) inashindwa kufundishwa katika jamii ya Waislamu?

Kulitokea nini?