Chuo cha dini ya Kiislam Madhehebu ya Ahlul Bayt (a.s) Mkoani Tanga, kijulikanacho kwa jina la Hawzatul Imam Qaim (a.s), kimetoa zawadi kwa wanafunzi walio faulu mitihani ya Nusu Mwaka kuanzia mwaka wa kwanza mpaka mwaka wa tano. Pia Chuo hicho kimetoa zawadi nono kwa wasomaji wa Qur'an Tukufu na kwa waliohifadhi Qur'an Tukufu aidha Chuo kimetoa zawadi kwa makundi yote yaliyofanya mitihani ikiwemo wanafunzi wa Madrasa kuanzia darasa la kwanza mpaka la kumi na moja kwa upande wa Wazee nao waliofaulu mitihani kwa kufikia 85/% na kuendelea nao pia wamepatiwa zawadi, pia chuo kimetoa zawadi kwa upande wa kina Mama wa nyumbani ambao wanasoma Madrasa katika chuo hicho, zawadi zimetolewa kuanzia mshindi wa kwanza hadi mshindi wa tano. Uongozi wa Hawzatul Imam Qaim (a.s) umewatunukia zawadi walimu kutokona na juhudi zao wanazozitoa katika kuelimisha wanafunzi na Umma kwa ujumla, mshindi wa kwanza na wapili katika mitihani iliyofanyika mwaka huu wamepata zawadi ya kwenda kufanya Ibada Tukufu ya Hijjah mwaka huu. Na Sheikh Taqee