HISTORIA FUPI KUHUSU HIZBULLAH.


KARIBU NDUGU MDAU KATIKA MAKALA HII MURWA UPATE UFAFANUZI WA YOTE HAYO YALIYOASHIRIWA HAPO JUU.
 

Hizbollah ni kundi la Muqawamah linaloundwa na (Mashia) wafuasi wa Ahlul-bait (a.s) wanaopatikana katika Jamii ya Lebanon.Kundi hili MWANZONI KABISA LILIUNDWA NA WANAHARAKATI WA KISHIA LAKINI KWA SASA LINAWAJUMUISHA WAPIGANIA HAKI WOTE WA KIISLAAM WA LEBANON MASHIA KWA MASUNII NA HATA WASIOKUWA WAASLAAM WA NDANI YA LEBANON PIA NI MEMBERS
WA HIZBULLAH.
Kwa sasa MUQAWAMAH WA HIZBULLAH unaongozwa na Sayyid Hasan Nasrullah ambapo ameshika jukumu la uongozi tangu mwaka 1992.Yeye ni Katibu mkuu wa Tatu wa Hizbullah,ambapo mwaka huo wa 1992 ameshika rasmi jukumu hilo baada ya utawala wa Israel kumuua KIGAIDI aliyekuwa Katibu mkuu wa Hizbullah zama hizo Sayyid Abbas al-Musawi.Mauaji hayo ya KIGAIDI yalitendwa tarehe 16February,mwaka 1992.
-------------------------------------
Kwa muhtasari: Hivyo Hizbullah ni sehemu ya Jamii ya watu wa Lebanon.Mashia nchini Lebanon,wanaunda asilimia 41 ya idadi mzima ya watu wa Lebanon.Na wapo kwa wingi katika maeneo ya matatu ya Lebanon ambayi ni:1-Kusini mwa Lebanon.2-Beirut na maeneo kadhaa yanayoizunguka Beirut,na Kasakazini mwa Bonde la Beqaa.3-Pamoja na Kanda ya Hirmil. Nchi hii ya Lebanon ilikuwa ikikaliwa kwa mabavu na ukoloni wa Ufaransa ambapo ilijipatia uhuru wake mwaka 1943,ikiwa ni tarehe 22 Novemba.Mkoroni huyu ((Ufaransa)) aliamua kuondoa Majeshi yake ya
uvamizi nchini Lebanon,mwaka 1946.
--------------------------------
Jamii ya Mashia nchini Lebanon ilianza kuwa na nguvu miaka ya 1960s na 70s,ambapo mwaka 1960 Imam Musa Sadr alikuja nchini Lebanon na akaongoza jamii ya Mashia katika mji wa Tyre.
Mwaka 1969 aliteuliwa rasmi kuwa mkuu wa kwanza wa Baraza kuu la Kiislamu la Shia.Mwaka 1974 alianzisha "Harakati ya Wanyonywaji wanyimwaji" ((Movement of the Deprived)) ili kuleta hali ya mbinyo kwa serikali ya wakati huo ikiwa lengo kuu ni kuleta hali nzuri na bora ya kiuchumi na kijamii kwa Mashia,wafuasi wa Ahlul-bait wa Mtume (s.a.w.w).
--------------------------------

HIZBOLLAH ILIUNDWA MWAKA GANI NA KWA MALENGO GANI:
----------------------------------
Israel iliivamia mara kadhaa Lebanon kiadui na kiuonevu,na historia imesajili kwamba mwaka 1978 katika Operesheni iliyoitwa:((Operation Litani)).Kisha ikaivamia tena mwaka 1982 na uvamizi huo wa kijeshi ulijulikana kama (Lebanon war) ambapo Utawala haram wa Israel ulidai kuanzisha vita hiyo kwa lengo la kuondoa PLO,nchini Lebanon.Na PLO maana yake: (Palestine Liberation Organization),kwa maana:((JUMUIA YA UKOMBOZI YA PALESTINA)).Jumuia hii wakati huo ilikifanya kazi zake ikiwa nchini Lebanon ikijaribu kuendesha harakati mbalimbali ili kuzikomboa Ardhi za Palestina kutoka katika makucha ya Utawala haram wa Israel.

Mapinduzi ya Kiislaam ya Jamhuri ya Kiislaam ya Iran ya mwaka 1979,yalileta athari kubwa sana na muhimu nchini Lebanon ambapo yalipandikiza moyo wa kujiamini kwa walebanon,wakawa na fikra ya kuunda Muqawamah kwa ajili ya kujihami wao,mali zao na nchi yao kwa ujumla dhidi ya maadui wa Kizayuni.Vyanzo vingi ninaashiria kuwa harakati hizo za kutaka kuwa na Muqawamah zilianza mapema mwaka 1982 na ilipofikia mwaka 1985 kikaundwa rasmi chombo cha kutetea haki za walebanon wanaoonenewa na kushambuliwa mara kwa mara na utawala haramu wa Isarel ambao wakati huo ulikuwa ukizikalia kwa mabavu ardhi za walebanon ambapo ulionyesha kutokuwa tayali kurudisha ardhi hizo kwa walebanon.

VYANZO RASMI VINASEMA:Hizbullah iliundwa na wafuasi wa Ragheb Harb,Kiongozi wa Muqawamah wa Mashia wa upande wa Kusini mwa Lebanon ambaye aliuliwa na utwawala wa Israel mnamo mwaka 1984 mwaka mmoja kabla ya kuazishwa Hizbullah. Kwa ufupi fikra na harakati za kuundwa kwa Hizbullah hazikuwa isipokuwa kutokana na uvamizi wa Israel nchini Lebanon mbapo ukaliaji wa mabavu wa ardhi za walebanon,uliwafanya walebanon kuwa na fikra pana nijinsi gani wataweza kumuondoa adui aliyewavamia na kuzikalia ardhi zao kimabavu.Na hapo ndipo Wana fikra wa Kiislaam wa lebanon,maadui wa uvamizi na dhulma walipounda chombo hiki kinachoitwa Kundi la Mwenyeezi Mungu (Hizbullah) ili kurudisha heshima ya Taifa lao la Lebanon na kumtimua adui vamizi. Kundi hili la Muqawamah lilipoundwa au lilipoanzishwa lilipata uungaji mkono kutoka sehemu mbalimbali zenye kupinga vita na uvamizi wa nchi fulani kwa nchi nyingine. Jamhuri ya Kiislaam ya Iran ndio Taifa pekee la Kiislaam lililotoa mchango mkubwa wa kifkra na uungaji mkono wa kimaada na kimaanawi kwa wanaharakati hao wa Hizbollah wanaopigania uhuru na heshima ya walebanon na Taifa zima la Lebanon. Hizbollah iliyoanza na idadi ndogo ya wanamapambano na wapigania haki ya Lebanon,sasa hivi imekuwa ni Jumuia kubwa mno ikiwa na viti kadhaa vya wabunge katika Serikali ya Lebabon,wakiwa na Redio Kituo cha Televisheni,huku wakiwa na mipango kadhaa ya maendeleo ya Kijamii. Jumuia hii ya Hizbullah kwa sasa ni Jumuia muhimu ndani ya Serikali ya Lebanon,na inapata sapoti kubwa sana kutoka kwa Jamii ya Mashia wa Lebanon,na imekuwa ni Jumuia yenye uwezo mkubwa wa kuitisha na kuhamasisha maandamano ya Mamia na Maelfu nchini Lebanon dhidi ya Utawala Haram wa Israel.

Hivyo,Hizbollah mbali na kuwa Muqawamah wa kutetea haki za walebanon na kuweka huru ardhi zao zinazokaliwa na wazayuni,pia ni moja wapo ya vyama vya Kisiasa nchini Lebanon vinavyoshiriki katika Serikali huru ya Lebanon.
---------------------
HIZBOLLAH NI KUNDI LA KIGAIDI AU LA?!.
Tumeelezea wazi malengo ya kuundwa kwa Hizbollah,hivyo si kundi la kigaidi kama makundi mengine yalivyo ya Kigaidi,bali ni wanaharakati na wanamuqawah wa Lebanon,ambao lengo lao kuu ni kuhakikisha wananchi wa Lebanon wanaishi kwa uhuru na amani pasina kubughudhiwa na wavamizi wa Kizayuni,na harakati zao zimeonekana katika ya hivi karibu (Vita ya mwaka 2006 na mwaka 2008) iliyoanzishwa na Israel dhidi ya Hizbullah ambapo Hizbullah imeweza kuhakikisha malengo yake ya kuasisiwa kwake kwa kurudisha ardhi za kusini mwa Lebanon zilizokuwa zimekaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel. Na huo ulikuwa ni ushindi mkubwa uliopelekea utawalaha haram wa Israel kuhaha na kulaumiana wao kwa wao kunatokana na kichapo walichokipata kutoka kwa wanamuqawamah hao wa Hizbollah. Ndio,kwa Isarael na kwa maadui wa Kiislaam. Hizbollah kwao litakuwa ni kundi la Kigaidi maana linapigana dhidi ya Israel na kuteteta haki za ndugu zao wa wapalestina,wanaodhulumiwa na ardhi zao kukaliwa kwa mabavu na Utawala haram na Ghasibu wa Israel.Hiyo ni kawaida kwa adui maana siku zote gaidi hajioni kama ni gaidi pindi afanyapo ugaidi,Isarel inafanya ugaidi si lebanon tu bali hata ndani ya Jamhuri ya Kiislaam ya Iran kwa kuua Maulamaa wa Nyuklia wa Iran,lakini hatujasikia ISRAEL ikisema mimi ni Gaidi au Marekani ikisema:Israel ni kundi la kigaidi,ama wale wanaotoka na kujitetea dhidi ya ugadi wa Israel ni kosa kubwa wanafanya kwa mtazamo wa watu hao wenye kudai kuiongoza dunia (masuper power wa dunia),kwa mantiki hiyo Hizbollah inatakiwa kukaa kimya na kuiachia Israel itawale itakavyo ardhi zao na kuikandamiza haki ya PALESTINA NA LEBANON,ama wakitoka kuonyesha upinzani na kupigana kwa kujihami dhidi ya maadui wa Taifa lao,basi zinakuja fikra za kwamba HIZBULLAH NI KUNDI LA KIGAIDI!!.VIPI MNAHUKUMU IKIWA KWELI NYINYI WAADILIFU?!.
------------------
HIZBOLLAH IMEKUMBWA NA UGAIDI,KUN AUSHAHIDI WOWOT EKUHUSU HILO?!.
------------------
Hizbullah ni moja ya watu waliokumba sana na ugaidi,mauaji ya hapa na pale ya kigaidi yanayotekelezwa na utawala haram wa Isarel yamekuwa ni mwiba kwa wanamuqawamah hawa wa Lebanon.Viongozi wengi wa Hzibollah wameuliwa kigaidi na utawala huu haram wa Israel,kuanzia mwasisi wa Hizbollah na wengine wengi.

Hivi karibu Israel imekiri wazi kumuua Kamanda Mughniya wa Hizbullah. Habari zinasema: Balozi wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Ujerumani amekiri kwamba Shirika la Kijasusi la Israel MOSSAD ndilo lililopanga na kutekeleza njama za kumuua Emad Mughniya kamanda wa Hizbullah Februari mwaka 2008 mjini Damascus,Syria.Avi Primor ameyaeleza hayo kwenye mahojiano na kanali moja ya televisheni nchini Ujerumani na kusisitiza kwamba, utawala wa Israel ndio uliotekeleza shambulio la kumuua kigaidi kamanda Mughniya. Hayo yanajiri katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel daima umekuwa ukikanusha kumuua Mughniya au kuhusika katika kupanga njama za kutekeleza shambulio hilo la kigaidi. Yote hayo yanafanyika na kuonwa na wanadunia,lakini hatujasikia hao wenye kuihami Israel wakisema chochote kunako ugaidi wa Utawala huo wa Israel. Twende Palestina:Huko nako Utawala huu umetekeleza mashambulizi kadhaa ya kigaidi dhidi ya viongozi wa Palestina na wapalestina,lakini tunalolisikia kutoka kwa wenye kuuhami utawala Ghasibu wa Israel ni hili kwamba:Muqawamah wa Palestina (HAMAS) ni kundi la kigaidi!!! kwa kuwa unaonyesha resistance na muqawamah dhidi ya Mayahudi wa Kizayuni wanaozikalia kwa mabavu ardhi zao.Basi ni nani gaidi na ni ipi maana sahihi ya Ugaidi ikiwa Israel sio Taifa la Kigaidi?!!.Je,kutetea haki zako na kuihami nchi yako na wananchi wa nchi yako ni ugaidi?!!.Mna nini nyinyi vipi mnahukumu?!!.

La kushangaza na kusikitisha ni kusikia baadhi ya waislaam tena wenye kudai wamesoma elimu safi ya dini ya Kiislaam wakidai kwamba:TUACHE KUITANGAZA AU KUZUNGUMZIA CHOCHOTE KUHUSIANA NA HIZBOLLAH MAANA MAREKANI IMESEMA NI KUNDI LA KIGAIDI?!!.Ni ajabu sana kusikia kauli kama hizo kwa watu ambao wengi tunatarajia kuwa wana akili na wamesoma na kuelimika,lakini inasikitisha kuona wamebeba nembo ya elimu katika jamii zetu kisha wanatoka na fikra za kwamba Marekani kaisha sema Hizbullah ni kundi la Kigaidi hivyo tuache kuzungumzia chochote kuhusiana na Hizbollah ati huenda Serikali ikamchukulia hatua mwenye kuizungumzia Hizbullah!!!
-----------
Binafsi nimekutana na watu hao wakibeba fikra hizo,siku tumia muda wangu kuwashangaa niliposikia wakizunguza fikra kama hizo zilizooza,isipokuwa nilichokifanya niliutumia muda wangu kuwauliza
maswali kadhaa kama ifutavyo; Niliwauliza hivi:Marekani ipo wazi kwamba ni maadui wa uislaam,hivyo
ikitokea siku wakasema hatutaki kuona waislaam wakiswali,ina maana pia mtasema kuwa tuache kuswali maana Marekani yuko dhidi ya swala na kaisha onyesha upinzani wake dhidi ya hilo?!.Au ikitokea Marekani akasema:Uislaam ni ugaidi(na kaisha sema kuhusu hilo!!) je,ni sahihi kwamba tuache kutangaza uislaam wetu wala kufanya Tabligh wazi wazi kwa kuwa Marekani kasema UISLAM NI UGAIDI?!.Mpaka leo sijapata majibu ya maswali hayo.Kuna watu wengine wamelewa Umarekani na Marekani kwao ni Mungu wa Pili.Allah (s.w) atuepushe na watu hao wenye kujua haki kupitia mitazamo ya Marekani na Magharibi.

Mwandishi wa Makala hii: Tzchalii.