IMAM HUSSEIN (A.S):


Imam Hussein (a.s) alitangaza kazi ya kuamrisha mema na kukataza maovu kama madhumuni ya harakati zake ambapo zilikuwa shuhuda kwa urithi wake. Wajibu huu mtukufu uko dhahiri kwenye sehemu mbalimbali katika simulizi za hotuba zake. Wakati alipokuwa anaaga kwenye kaburi la babu yake, alisema:
"Ewe Allah! Hili ni kaburi la Mtume wako (s.a.w.w) na mimi mjukuu wa Mtume wako Muhammad (s.a.w.w). Nakabiliana na jambo ambalo unalijua vizuri zaidi kuliko mimi. Ewe Allah! Nayapenda maadili mema na nayachukia maovu."
Rejea: Mawassae Kalematul Imam Hussein, Uk. 278