MAADILI:

Maadili ambayo yamerejea kwenye uhai kwa matokeo ya kuasi kwa Imam Hussein (a.s) hutajwa kama ifuatavyo: Maadili ya Ashura na Maadili ya Hussein (a.s). Kabla ya kujadili maadili haya ni muhimu kwanza kuelewa madhumuni ya mihanga hii mikubwa ilikuwa ni nini. Tukio hili la msiba limekuwa kwenye ndimi zetu tangu karne nyingi na mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusiana nalo. Ni vizuri kumuuliza mtangulizi, Kiongozi mwenyewe wa mashahidi, kuhusu madhumuni ya kadhia hii kuliko kuyaendea maoni na maandishi ya wachambuzi mbalimbali, waandishi, watafiti mahatibu, wanachuoni na wasomi, ambao wameelezea mitazamo yao juu ya kadhia hii. Lazima tutafakari juu ya maneno ya Imam Hussein (a.s) ili kuona kile alichosema kuhusiana na madhumuni ya kuasi kwake. Wakati wa kuondoka Madina, kwa mikono yake mitukufu, Imam Hussein (a.s) aliandika wosia wa urithi kwa ajili ya ndugu yake Muhammad bin Hanafia (a.s) na akamkabidhi.
Katika wosia huu wa urithi anaelezea madhumuni ya kuasi kwake:
"Siondoki (kutoka Madina) kama muasi, makandamizaji na dhalimu, bali madhumuni yani ni kuutengeneza Umma wa babu yangu. Njia pekee ya kufanya mageuzi haya ni Amr Bil Ma'ruf (kuamrisha mema, kwenye Maadili yajulikanayo) na Nahi Anal Munkar (Kukataza maovu), yaani, nataka kuutengeneza Umma kwa njia ya Amr Bil Ma'ruf na Nahi Anal Munkar. Sio kwamba mimi ni mtu wa kwanza ambaye ninafuata njia hii ili kuutengeneza Umma, kabla yangu mimi babu yangu na baba yangu wote walifuata njia hii tu. Nami pia nataka kufuata mwenendo wao wa kufanya Amr Bil Ma'ruf na Nahi Anal Munkar kwa ajili ya kuutengeneza Ummah."
Unaweza kurejea: Mawassai Kalimatul Imam Hussein Uk. 290 - 291