Chuo cha dini ya Kiislamu kinachotambulika kwa jina la Abil Fadhlil Abbas (a.s) kilichopo Morogoro, walimu na wanafunzi wameamua kushirikiana katika kilimo cha Mbogamboga,Mpunga pamoja na Mahindi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika chuo chao, mwalimu wa chuo hicho ndugu Abuu Hamza Said amesema kuwa wameamua kupambana na changamoto zinazowakabili katika chuo hicho kivitendo kwani Umasikini ni kikwazo kikubwa katika kufikia malengo, ndugu Abuu Hamza amewataka Waumini wa dini ya Kiislamu kuwaombea dua ili waweze kufanikiwa katika shughuli yao ya kupambana na umasikini kupitia kilimo wanachokiendesha hivi sasa. Huu ni mfano mzuri kwa kila anayefanya kazi ya kuitumikia jamii katika masuala ya malezi lazima tuwe na fikra huru za kutuendeleza katika mambo yetu.