WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WA MADHEHEBU YA SHIA WASWALI SWALA YA EID IFTRI KATIKA UWANJA WA PIPO KIGOGO POST.

Swala ya Eid Fitri kitaifa imeswaliwa leo katika uwanja wa Pipo Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, Sheikh Hemed Jalala Kiongozi wa harakati za Kiislam Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah Tanzania na Imam Mkuu wa Msikiti wa Madhehebu ya Shia Kigogo, amewataka Waumini wa dini ya Kiislam kuachana na matendo ya kukufurishana na kupeana majina mabaya kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea mifarakano katika jamii aidha Sheikh amesema kuwa kitendo cha kumkufurisha mtu ni kumnyang'anya haki yake ya kibinadamu kwa sababu mwanadamu anayo haki ya kuishi na heshima hivyo unapomwambia kafiri unakuwa umemwambia hana dini umemwambia damu yako ni halali hivyo ni hatari.
Sheikh amewataka Waumini hao watambue kuwa itakapo dhihiri katika jamii wa watu wa aina yeyote tabia ya kukufurishana licha ya kuondoa haki za kibinadamu bali kuna hatari kubwa inayoikabili jamii iliyokuwa na tabia ya kuitana majina mabaya na kukufurishana na kutoana katika dini hatari kubwa ni hatari ya jamii kuanza kugawanyika inaanza kuwa makundi makundi kundi moja linamwambia yule ni kafiri na jengine linamwambia mwingime ni kundi la Bida'a nakufikia hata kuitana Wanafiki tayari kutakuwa na mgawanyiko katika jamii, Kafiri na Muislamu utawawekaje katika kiti kimoja kafiri ni mwanadamu asiyekuwa na dini na mwanadamu mwenye dini wapi utaweza kuwaweka katika meza moja, jamii yeyote itakapoanza kufarikiana nakutokuweza kukaa pamoja kuzungumza mambo yake jamii hiyo itambulike kuwa ni jamii maiti, Sheikh amewataka Waumini hao wasije wakawa na tabia ya kuvutana na kufarakana wakishafikia katika kufarakana watafeli katika mambo yao watashindwa kufikiria mambo muhimu katika jamii yao kwa sababu ni jamii iliyogawanyika jamii yeyote ambayo wataalamu wake na wasomi wake hawakai katika meza moja hakuna kitakachoendelea katika jamii yao, jamii ya Watanzania ni jamii ya watu waliyokaa kwapamoja miaka mingi ni jamii ambayo haijui kukufurishana ndio maana ukiisoma historia ya nchi ya Tanzania Masheikh na Waislamu pamoja na Maostadh wanamchango mkubwa katika kuhakikisha nchi ya Tanzania imekuwa uhuru na katika kuutafuta uhuru wa nchi ya Tanzania walikaa Waislamu na Wakristo meza moja kutafuta uhuru wa Tanzania hawakuwa na fikira za kukufurishana wala za kutuhumiana na kupeana majina mabaya na nchi ya Tanzania ikawa uhuru na salama, Wazee waliyokuwa Waislamu na wasio kuwa Waislamu walikaa meza moja ndio haya maelewano mazuri yaliyokuwepo katika aridhi ya Tanzania yanayoonekana leo amani iliyokuwepo leo Watanzania hatujui kubaguana dini zetu tofauti lakini sote ni kitu kimoja kwa sababu Wazee wetu wa mwanzo hawakuwa na fikra za kukufurishana wala zakupeana majina mabaya na majina ambayo hayafai wakakaa meza moja leo tunafaidika na utulivu tuliyokuwa nao na amani tuliyonayo, amemaliza kwa kusema kuwa fikra za kukufurishana na kupeanza majina mabaya katika jamii yetu kama zitaendelea tujue kuwa hakuna maendeleo yeyote yatakayoletwa na Waislamu watambue kuwa kufeli ndio kutakapo wakabili watashindwa kukaa kufikiri kuwa kama kuna mambo muhimu ya kuhitajia katika jamii yao ikiwemo elimu, afya pamoja na tiba hayo yote yatashindwa kupangika mwisho wake wataingia katika kugaiana pepo na moto wewe unakwenda motoni wewe unakwenda peponi, sio kazi yetu kugawa pepo na moto hapa duniani sisi ni wajibu wetu kutenda kama Waislamu kukaa katika meza moja kuangalia ni mapungufu gani yanayotukabili katika jamii ya Kiislamu kitu gani hatuna, hatari ya kukufurishana ni hatari mbaya sisi kama Waislamu lazima tuungane tunapompata mtu yeyote au kikundi chochote malengo yake na itikadi zake pamoja na fikra zake ni kuwakufurisha watu wengine sisi kama Waislamu lazima tuungane na lazima tuwe pamoja kumpiga vita mtu huyo au kukipiga vita kikundi hicho kwa sababu hakiutakii heri Uislamu na Waislamu pamoja na jamii ya Watanzania.