SAFARI ZA HARAKATI ZA UJUE USHIA MIKOANI KWA MARA YA KWANZA CHINI YA UONGOZI WA SHEIKH HEMED JALALA.

Muhadhara wa UJUE USHIA kwa mara ya kwanza ulianzia Mkoani Tanga wiliya ya Lushoto huko Mlalo mwaka 2012 chini ya Uongozi wa Sheikh Hemed Jalala, kazi hiyo ilileta muamko mkubwa mno kwa wafuasi wa dini ya Kiislam Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah pamoja na Madhehebu ya Sunni, ilipofika tarehe 17/06/2012 Uongozi wa harakati za UJUE USHIA chini ya Sheikh Hemed Jalala ulifanikiwa kuitisha mkutano mkubwa wa Mashia wanaoishi Dar es Salaam kwa ajili ya kutambuana na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Kishia Tanzania.
Tunaweza kuona ni kwa mda mchache sana jamii ya Kishia iliweza kutembea katika sehemu mbalimbali na kufikisha ujumbe halisi wa dini ya Kiislam aliyouacha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), tunajukumu kubwa la kuitunza kazi hii iliyoanzishwa na waasisi hawa. Tusikubali hata siku moja mtu atushawishi kuivunja kazi hii ambayo imetuletea heshima katika jamii yetu.