Hakika uboreshaji wa hotuba za kidini kwa ajili ya maslahi ya binadamu, sio matakwa kwa ajili ya ukamilifu wake, na wala sio jambo la kijuu juu, bali ni jambo lenye umuhimu wa hali ya juu, jambo ambalo liko katikati ya mambo yanawahusu watu na wanalolihitaji mno, Kwa kweli jambo hili ni njia inayothibitisha kupatikana mambo ya kimsingi, ambayo watu wamechelewa sana kuyapata, miongoni mwayo ambayo ni muhimu zaidi ni kama yafuatayo:
KWANZA: Kuhakikisha upatikanaji wa maendeleo ya kibinadamu katika jamii zetu, kwani leo binadamu anaishi katika hali mbaya, akiwa anakosa mbinu ya kujenga maisha bora, na kukosa kustarehe na haki zake za kibinadamu kwa mujibu wa sheria.

PILI: Kuwa na mafungamano pamoja na wengine ndani ya Umma na ndani ya nchi, na pia nje ya nchi pamoja na watu wengine na tamaduni mbalimbali, kwani jamii zetu zinasibiwa na tatizo la kuwepo mafungamano na vikundi vingine vya watu, kwani Umma umeingizwa katika vita vyenye kulenga kuwazuia kuamiliana pamoja na tamaduni nyingine na mataifa mengine kwa sababu ya ugaidi.
TATU: Kuchangia katika kuhudumia masuala ya kibinadamu katika kiwango cha ulimwengu, ili Umma uwe sambamba na yale yanayolinganiwa na Uislamu, kama vile tabia njema, mafunzo na kaulimbiu za ujumbe wake Mtukufu.
Hakika Qur'an Tukufu inautangaza Uislamu kuwa ni dini inayojishughulisha na mambo ya kibinadamu kwa ujumla, inasema: "Na hatukukutuma ila kwa watu wote...." (Qur'an 34:28).
Na ujumbe, rehema na amani ni kwa mataifa yote ulimwenguni, inasema:
"Na hakukutuma ila uwe ni rehema kwa walimwengu wote."
Na Umma wa Kiislamu unapaswa kuwa ndio muongozaji wa mambo mema katika jamii yote ya kibinadamu, kama Qur'an inavyosema:
"Mmekuwa ni Umma bora uliotolewa kwa watu..."
Basi hakuna budi kutolewa hotuba zenye kuelekeza majukumu haya, na kuutangaza Uislamu katika ulimwengu katika nafasi hii. Na Sheikh Hassan Musa al-Saffar