Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, harakati hiyo itaendelea kuiunga mkono Syria mkabala na magaidi wa kitakfiri. Sheikh Naim Qassem amesema hayo leo kwenye hotuba yake mjini Damascus katika mkutano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi wa kitakfiri na kubainisha kwamba, Hizbullah itaendelea kuiunga mkono Syria na kwamba, kila mahala itakapohitajika haitasita kwenda na kutoa msaada unaohitajika. Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameongeza kusema kuwa, njia ya utatuzi wa mgogoro wa Syria inapaswa kuwa ya kisiasa na iwe ni baina ya wananchi wenyewe wa nchi hiyo. Amesema, kama Hizbullah itashindwa kulinda ardhi na mamlaka ya kujitawala Syria basi haitakuwa rahisi kwake kulinda ardhi ya Lebanon. Sheikh Naim Qassem amessitiza kuwa, magaidi wa kitakfiri wameletwa na Marekani na wanaishi kwa pesa za mafuta za nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na kwamba nchi hizo ndizo zinazowapatia suhula na zana mbalimbali matakfiri hao ili wawe na udhibiti nchini Syria; lakini hata hivyo wameshindwa kufikia lengo hilo. Aidha Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema, Saudia inatenda jinai za karne huko Yemen na kuwa hakuna tofauti yoyote baina ya Israel, Saudia na Marekani. Fuatila habari za kina kwa kubofya link hii:http://kiswahili.irib.ir/…/50370-hizbullah-tutaendelea-kuiu…
SWADDIQI: US INATAKA KUZIGAWA NCHI ZA MASHARIKI YA KATI.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na mwenendo wa usalama katika Mashariki ya Kati na kuituhumu Marekani kwamba, inafanya njama za kuzigawa nchi za eneo hili. Sheikh Kazem Seddiqi amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa mjini Tehran na kusisitiza kuwa, Marekani inafuatilia kuzigawa nchi za Syria, Iraq na Yemen na kwamba, Washington inafanya dhulma yote hii na udanganyifu wote huu kwa shabaha ya kutoa himaya na uungaji mkono kwa utawala haramu wa Israel. Hujjatulislam Walmuslimeen Seddiqi amebainisha kwamba, daima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikiziunga mkono serikali zilizoingia madarakani kwa kura za wananchi na kuongeza kuwa, fitina na hila za Marekani zimezifanya nchi za Kiislamu katika Mashariki ya Kati kukabiliwa na mgogoro. Ameongeza kuwa, hatua ya Marekani ya kuzipatia silaha tawala zisizo za wananchi zimelifanya eneo hili kukumbwa na ukosefu wa usalama na amani. Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, ili mataifa ya Kiislamu yaweze kukabiliana na njama za Marekani na Wazayuni katika Mashariki ya Kati zinapaswa kuimarisha umoja na mshikamano baina yao.