Viongozi wa Cameroon wamesema kuwa marufuku iliyokuwa imewekwa kwa vazi la hijab nchini humo itaendelezwa. Duru rasmi leo zimetangaza kuwa viongozi wa Cameroon wameamua kuendeleza marufuku iliyokuwa imetangaza awali kwa vazi la hijaab la burqa na niqaab katika maeneo ya mashariki na pwani ya nchi hiyo kwa kisingingizo cha kuzuia hatari ya mashambulizi nchini humo. Viongozi wa Cameroon wamechukua uamuzi huo baada ya kujiri mlipuko uliouwa watu 13 na kujeruhi wengine 31. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, marufuku hiyo inajumuisha ushonaji, uuzaji na uvaaji wa vazi la burqa na kwamba maimamu wa misikiti pia watapaswa kusimamia vikali mavazi hayo. Hatua za kiusalama pia zimeimarishwa katika barabara zinazoelekea katika miji mikubwa ya Cameroon ukiwemo mji mkuu wa nchi hiyo Yaounde na ule wa Douala.http://kiswahili.irib.ir/…/50367-serikali-ya-cameroon-kuend…