WAUMINI wa Dhehebu la Shia Ithna asheri, Kanda ya Ziwa, Mkoa wa Mwanza, wameliomba Baraza Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA), Liwashirikishe kwenye mchakato wa kumchagua Mufti Mkuu wa Tanzania uliyopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Dhehebu hilo pia limepongeza uteuzi wa Kaimu Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi na kumwomba azingatie ombi lao la kushirikiana katika mchakato huo na masuala yote yanayowahusu Waislamu. Ombi na pongezi hizo zimetolewa jana na Mwenyekiti wa Bilal Muslim Mission of Tanzania, Kanda ya Ziwa, Sibtain Meghjee, alipozungumza na gazeti hili akisisitiza kuwa, wana imani kubwa na Sheikh Zuberi wakiamini atawaunganisha Waumini wa dini zote za Kiislamu ili kuondoa dhana ya ubaguzi, migogoro miongoni mwao.
''Waislamu wa Dhehebu la Shia Ithna asheri, wana matumaini makubwa na Sheikh Zuberi wakiamini kipindi hiki ambacho anakaimu nafasi ya Mufti Mkuu, atawaunganisha Waislamu wote kupitia madhehebu yao ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Mufti Mkuu," alisema.
Alisema Uchaguzi wa Mufti Mkuu umekuwa ukihusisha Waislamu wa dhehebu la Suni pekee wakati kuna madhehebu mengi ambayo ni Shia, Bohora, Ismailia na Ibadhi ambayo huachwa nje ya mchakato huo.
Meghjee alisema ili kuondoa changamoto ya migogoro, misuguano isiyo na tija miongoni mwa waumini wa dini za Kiislamu, kudumisha amani, utulivu na mshikamano nchini, Sheikh Zuber anapaswa kuliona hilo na kuwashirikisha katika uchaguzi huo.
Aliongeza kuwa, waumini wa dhehebu hilo watampa ushirikiano ili aweze kudumisha amani na utulivu wa nchi kwa kupinga dhuluma, uonevu, unyanyasaji, ukandamizaji, upendeleo wa aina yoyote. Chanzo cha habari: Majira gazeti la UHURU la kila siku la tarehe 15 July 2015 ukurasa wa 3
Mwandishi: Daud Magesa, Mwanza.