UBAGUZI DHIDI YA WAISLAMU WAONGEZEKA NCHINI CZECH.

Waislamu katika Jamhuri ya Czech wameeleza wasiwasi wao kutokana na kushadidi kwa vitendo vya ubaguzi dhidi yao na dhidi ya wahajiri Waislamu nchini humo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo imeonya juu ya kuongezeka kwa vituo vinavyoendesha harakati dhidi ya wahajiri na Waislamu wa taifa hilo na kuelezea wasiwasi wake kuhusiana na suala hilo. Kwa mujibu wa wizara hiyo, viongozi wa vituo hivyo wamekuwa wakiwashawishi viongozi wa mrengo wa kulia kwa lengo la kushadidisha mashinikizo na ukandamizaji dhidi ya wahijiri na Waislamu. Hivi karibuni shirika la STEM, lilitoa ripoti ya uchunguzi wake wa maoni kwamba, idadi ya Waislamu katika Jamhuri ya Czech inazidi kuongezeka siku hadi siku.
Kwa upande wake Vladimir Sanka, mkuu wa Kituo cha Kiislamu mjini Prague, amesema kuwa, idadi ya Waislamu inazidi kuongezeka katika Jamhuri ya Czech, na ndio maana baadhi ya vyombo vya habari na makundi yenye chuki, yakazidisha harakati zao za kibaguzi dhidi ya Waislamu.


WAISLAM NIGERIA WAPINGA MARUFUKU YA HIJABU.

Waislamu nchini Nigeria awamepinga mpango wa kupiga marufuku vazi la hijabu nchini humo na kusimamishwa na kupekuliwa wanawake wanaovaa vazi la staha la hijabu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Jama'atu Nasril Islam (JNI), ya Nigeria, Khalid Abu Bakar amesema kundi hilo halikubaliani na marufuku ya vazi la hijabu na kuongeza kuwa, siasa za ketenganisha watu na kuwapekua wanawake wenye vazi la hijabu kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi ni kielelezo cha ukandamizaji kwa misingi ya itikadi za kidini.
Khalid Abu Bakar amesema, mwanadamu yeyote hana hatia mpaka ithibitike kinyume chake na kwa msingi huo amelaani mpango wa askari usalama wa kuwapekua wanawake Waislamu wanaovaa vazi la hijabu. Amesisitiza kuwa hatua hiyo ni ya kibaguzi na haitasaidia kupata suluhisho la kimsingi la tatizo la ugaidi.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa taasisi ya Umma wa Waislamu ya kusini magharibi mwa Nigeria, Daud Nuwaibi, amesema dunia ya leo inatumia mbinu za kisasa za kuzuia uhalifu na kwamba kuwapekua wanawake Waislamu kwa sababu ya vazi lao la hijabu ni makosa makubwa.
Maafisa wa usalama wa Nigeria wanatetea hatua hiyo wakidai kuwa watu wanaojilipua kwa mabomu wamekuwa wakitumia vazi la hijabu kuficha uhalifu huo.


Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamefanya maandamano kupinga muswada uliowasilishwa na Rais Catherine Samba-Panza wa nchi hiyo, unaowazuia raia wa taifa hilo walioko nje kutoshiriki kujiandikisha wala kupiga kura katika uchaguzi ujao. Kwa mujibu wa waandamanaji, muswada huo, unalengo la kuwazuia Waislamu ambao ndio wengi walioko nje, kutoshiriki katika zoezi hilo ambalo ni haki yao ya msingi.
Tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati, Mosi Mwasi kwa taarifa zaidi…bonyeza hapa chini…………/ http://kiswahili.irib.ir/habari/mahojiano/item/50197-waislamu-car-wataka-raia-walioko-nje-ya-nchi-wapige-kura-kama-wenzao-walioko-ndani