VIKOSI VYA MAJESHI YA KISHIA VYAENDELEZA MASHAMBULIZI DHIDI YA DAESH IRAQ.

Vikosi vya majeshi ya Shia ya Iraq vimeendelea kufanya mashambulizi mazito dhidi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wanaoudhibiti mkoa wa Anbar, mapaka kufika sasa wanajeshi wa kishia wamefanikiwa kuwakamata magaidi 700 wa Daesh ambao wanasadikiwa kuwa ni raia wa kigeni.
Wanajeshi wa kishia ambao wameombwa msaada wa uokozi na viongozi wa kidini wakisunni wa mkoa huo wa Ramadi.
Wanajeshi wa kishia bila ajizi wamekubali ombi za ndugu zao masunni na kwenda kuwaokoa kutoka mikononi mwa magaidi hao wa Daesh.
Wanajeshi wa Shia ambao wanapata mafunzo na misaada ya kijeshi kutoka kwa jeshi la Quds la jamhuri ya kiislamu ya Iran, wameshinda vita vingi dhidi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh, na kusabibisha kundi hilo la kigaidi kukimbia maeneo mengi ya Iraq.
Wapiganaji wakishia  wameiita Oparesheni hiyo kwa jina la "Labaik ya Hussein" ambayo tafsiri yake ni "Tuko kwa ajili yako Ewe Hussein". Wakiamaanisha Imam Hussein ambaye ni mjukuu wa mtume Muhammad s.a.w, ambaye mama yake ni Fatma bint wa mtume Muhammad na baba yake ni Ali bin abi Twalib ambaye alikuwa ni ndugu wa mtume na swahaba shujaa na mwenye elimu ya juu.
Mjini Washington, msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, Kanali Steven Warren, alisema kuchagua jina  la kimadhehebu zaidi kwa operesheni ndani ya ngome ya Wasunni nchini Iraq haikuwa jambo la busara.
Kauli ya msemaji wa Marekani inaonekana kuwa ni ya uchochezi kwani Imam Hussein si mtu anayeheshimiwa na mashia pekee bali anaheshimiwa na waislamu wote kwa ujumla.