Matatizo yaliko ndani
ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran baada ya Mapinduzi ya Kiislam yenyewe ni
somo tosha; tena yote haya yanahusika kwenye ukweli kwamba Mapinduzi ya
Kiislam yalolenga na kuweka juhudi katika kutekeleza Mfumo wa Wilaya. Ni
lazima idhihirike watu kwetu sisi kuhusu njama za mipango ya maadui wa
Mapinduzi na dini, zile mamlaka zenye
kiburi zilizonayo juu ya Iran; na wanashughulika kivitendo juu ya
mipango hii. Kama unavyoweza kuona baadhi ya mambo kwa uwazi kabisa,
kuna uingiaji mkubwa wa bajeti ya Kimarekani kwa ajili ya kueneza
uharibifu wa tamaduni miongoni mwa watu, na hilo nalo hususani ni kwa
vijana. Mamilioni ya dola za Kimarekani yanasambazwa ili kuwavuruga
vijana wa Iran na kuwachochea dhidi ya Mfumo wa Wilaya, kuwaingiza
wanawake wa Kiirani kwenye utovu wa staha na upujufu, kuwafanya vijana
wa Iran kuwa waathirika wa madawa ya kulevya, kueneza maelezo ya matusi
ya kingono na lugha chafu; yote haya yanafanywa na bajeti ya baraza la
Congress la Marekani mahususi na iliyotamkwa wazi hadharani kwa ajili ya
opresheni za siri siri ndani ya Iran. Mbali na hii, bajeti isiyotamkwa
hadharani ni kubwa zaidi kuliko ile iliyotamkwa katika kueneza
mmomonyoko wa maadili ndani ya Iran. Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi