WAISLAMU WA MADHEHEBU YA SHIA ITHNA ASHARIYYAH WA SWALI SWALA YA EID KATIKA KIWANJA CHA PIPO, KIGOGO POST, JIJINI DAR ES SALAAM.

Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah leo wameswali swala ya Eid Al-Adha kitaifa katika Kiwanja cha Pipo kilichopo Kigogo Post jijini Dar es Salaam, Khatibu wa Swala ya Eid amewataka Waumini wa Kiislam kuwa na Taqwa amesema bila ya Taqwa hakuna Uislamu, mambo yeyote katika jamii ikikosekana Taqwa jamii hiyo haiwezi kufanikiwa pia amesema ni muhimu Waislam kuwa kitu kimoja kwa kuwa Ibada Tukufu ya Hijjah ni Ibada inayowakusanya watu bila kuangalia rangi wala makabila kwa hiyo ni vyema waislam kuungana na kushirikiana katika kila jambo na kuweka mbali tofauti zao.