KIONGOZI MUADHAMU ARUHUSIWA KUONDOKA HOSPITALI.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei leo asubuhi ameruhusiwa kuondoka hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate) siku kadhaa zilizopita.
Habari kutoka Ofisi ya Kiongozi Muadhamu zinasema ameruhusiwa baada ya kupata nafuu kikamilifu.
Tarehe 8 Septemba Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alifanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate) katika operesheni iliyofanyika kwa mafanikio katika mojawapo ya hospitali za umma mjini Tehran.
Wakati huo mkuu wa timu ya madaktari wake alisema kuwa kupona kabisa kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa aina hiyo kunahitaji siku tatu hadi tano. Dakta Alireza Marandi alisema kuwa, upasuaji huo ulichukua muda wa chini ya nusu saa na ulifanywa kwa kutumia ganzi isiyokuwa ya mwili mzima (local anesthesia). Chanzo cha habari:http://kiswahili.irib.ir/habari/kiongozi/item/43064-kiongozi-muadhamu-aruhusiwa-kuondoka-hospitali