Abdul Aziz Abdullah Aal
Sheikh, Mufti wa Saudi Arabia na Mkuu wa Kamati ya Maulama wa nchi hiyo
amesema kuwa, kufanya maaandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina wa Gaza
ni hatua ya kuleta vurugu na isiyo na faida. Matamshi hayo ya
kustaajabisha yamekuja wiki moja baada ya Swaleh al-Haidan, Mwenyekiti
wa Baraza Kuu la Mahakama la Saudia kutoa fatuwa
ya kuharamisha maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina. Al-Haidan
ameongeza kuwa, kufanya maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina ni sawa
na kufanya uharibifu katika ardhi. Hii ni katika hali ambayo mamilioni
ya Waislamu na hata wasio kuwa Waislamu wamejitokeza kote duniani katika
maandamano ya kulaani jinai za Israel dhidi ya Ghaza. Waziri Mkuu wa
Utawala wa Kizayuni amekiri kuwa maandamano hayo yametoa pigo kubwa kwa
itibari ya utawala huo kimataifa. Pamoja na hayo wanazuoni hao wa Saudia
wamepinga maandamano hayo.
Wiki iliyopita mwanaharakati mmoja wa
Saudia alitangaza kuwa kuwa wawala wa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za
Kiarabu (Imarati) mbali na kuipatia Israel msaada wa kifedha kuvamia
Ghaza kwa njia ya nchi kavu pia walimuahidi waziri mkuu wa utawala wa
Kizayuni Benjamin Netanyahu kuwa, iwapo atakamilisha ipasavyo hujuma
dhidi ya Ghaza na kuangamiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya
Palestina Hamas, basi nchi hizo mbili zitaurushusu utawala wa Kizayuni
ufungue balozi zake Riyadh na Abu Dhabi.