Anasema Imam Hasan (a.s):
"Je mnajua (Tawadhui) unyenyekevu ni nini?!.
Unyenyekevu ni wewe kutoka nyumbani kwako na hukutani na muislam yeyote ispokuwa utamuona ni mwenye fadhila juu yako".
Ndugu msomaji unayeisoma meseji hii kwa muda huu ni kwamba:Yeyote mwenye kibri siku zote ni mtu duni,dhalili, na hana hadhi yoyote hata kama atajiona nafsi yake yupo juu zaidi ya watu wote.
Na mwenye kunyenyekea siku zote yupo katika daraja ya juu na ni mwenye hadhi kubwa na utukufu hata km watu watamuona ni mtu duni asokuwa na hadhi.
_________
Mshairi anasema:
KUWA MNYENYEKEVU ILI UWE KAMA (((NYOTA))) INAYOMWANGAZIA MTU MWENYE KUTIZAMA JUU YA USAWA WA BAHARI (((HUKU IKIWA JUU NYOTA HIYO))),NA USIWE KAMA VILE (((MOSHI)))
UNAOJIPANDISHA JUU KABISA KATIKA TABAKA ZA ANGA HUKU (((MOSHI HUO UKIWA CHINI KABISA))).
_________
Ndugu msomaji unaendelea kuisoma makala hii fupi: Tambua kuwa zama hazigandi ktk hali moja kama Allah (s.w) alivyosema:
"و تلک الأیام نداولها بین الناس"
"Na siku za namna hii tunawaletea watu kwa zama1".
_______
1- Surat Aali Imraan:Aya ya 140.
_______
Kwa maana:Mara inatujia hali ya ufakiri na umaskini,mara unatujia utajiri,mara utukufu,mara udhalili,mara cheo ....n.k.
Mwenye kufaulu na kupata saada ni yule atakaye dumu ktk ((asili moja)) kwa kila hali tulizoziashiria,nayo ni:
(تقو الله عز وجل والتواضع علی کل حال).
Kumcha Allah (s.w) na kuwa mnyenyekevu ktk hali zote.
Kila muislam atambue kuwa Unyenyekevu na Ucha_Mungu ni ktk Akhlaq na tabia njema za Mitume na Manabii pamoja na watu wema.Ni uzuri ulioje kujipamba kwa sifa waliojipamba nayo Manabii na Mitume wa Allah (s.w) Rehma na Amani ziwe juu yao.
Rabi upe nguvu Uislam na Waislam,na idhalilishe Shirki na washirikina.
Wassalam Alaikum Warahmatullah wabarakatuh.
____________
Mwandishi wa makala hii ni:Sheikh Taqee.