MSIKITI WA MTAMBANI ULIYOPO WILAYA YA KINONDONI WATEKETEA KWA MOTO.


Msikiti wa Mtambani uliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam umeteketea kwa moto usiku wa tarehe 13/08/2014.
Waumini wa Kiislam na vijana waliyokuwa katika tukio hilo wamefanikiwa kuuzima moto wakishirikiana na Kikosi cha zima moto huku jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi mkali, katika harakati za kuukomboa Msikiti baadhi ya vijana walipata majeraha na wengine kushonwa sehemu za kichwa kutokana na Vioo vya madirisha kuanguka hovyo katika eneo la Msikiti huo.