Zaidi ya
miaka 60 tangu kuanzishwa utawala wa Israel mnamo May, 14, 1948 udhalimu wakina
umekuwa ukiendelea. Wakimbizi wa Ki-Palestina ndio idadi kubwa kushida yote ya
wakimbizi iliyobakia duniani.
Wapalestina Millioni
1.3 wanaishi nchini Israel kama “Raia wa Israel,” lakini licha ya hadhi yao
kama raia, bado wanakumbwa na ubaguzi wa kimfumo hatua kwa hatua. Wengi wao
wanakatazwa kuishi kwenye vijiji na makazi yao ambamo walifukuzwa kikatili, na mali
zao zimekamatwa kwa ajili ya matumizi ya Kiyahudi tu. Katika Istilahi za
Orwellian, sheria za Israel zinawaonyesha wakimbizi hawa wa ndani kama “wasiopo
wakati huu” (Present obsentees)
Mnamo mwaka
1967 Israel ilianzisha vita vyake vya tatu na wakatwaa ardhi zaidi ya
Wapalestina (na ya Waarabu wengine). Israel pia ilishambulia meli ya kivita ya
Marekani, “The USS Liberty,” ikiwauwa na kujeruhi zaidi ya Wamarekani 200,
tukio ambalo linabakia kufunikwa kabisa leo hii, licha ya juhudi za kundi
lisilo la kawaida la maafisa wa ngazi ya juu wa kijeshi watumishi wa kiraia za
kulifichua na kuliweka wazi.
Israel iliukalia
Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza asilimia 22 ya mwisho ya mamlaka (iliyokadiriwa)
ya Palestina na ikaanza kujenga makazi ya Waisrael wa Kiyahudi kwenye ardhi
iliyoporwa kutoka kwa Waislam na Wakristo wa Kipalestina. Imebomoa zaidi ya
makazi 24,145 ya Wapalestina tangu mwaka 1967. Mwaka 2005 Israel ilirejesha
ardhi ya Gaza kwa wenyewe, lakini inaendelea kudhibiti mipaka yake, bandari na
eneo la anga, na kuigeuza Gaza kama gereza kubwa, ambamo watu Million 1.5
wanashikiliwa chini ya kile kinachoelezwa na kamisheni ya haki za Binadamu ya
umoja wa Mataifa masharti ya “Kimsiba.”
Zaidi ya
Wapelestina 7,000 Wanaume, Wanawake na watoto wamefungwa katika magereza ya
Israel chini ya hali ya kudhalilishwa kimwili (Wengi wao wala hawakushitakiwa
kwa uhalifu wowote) na haki za msingi za kibinadamu za Wapalestina wote chini
ya utawala wa Israel kwa kawaida zikikiukwa. Baadhi ya wafungwa waliopewa
mateso na Israel walikuwa ni raia wa Marekani. Katika ukatili ambao ulianza
2000, kupitia Feb. 5, 2009, majeshi ya Israel yaliuwa Wapalestina 6,348;
Vikundi vya upinzani vya Palestina viliuwa Waisrael 1,072. Jeshi la Israel, la
nne lenye nguvu sana duniani linamiliki mamia ya silaha za nyuklia.