Swala ya Eid Fitr iliyoswaliwa Kigogo, jijini
Dar es Salaam. Imam wa swala ya Eid Sheikh Hemed Jalala amewataka
Viongozi wa dini kutoruhusu sehemu za ibada kuwa chanzo cha uvunjifu wa
amani nchini pia imam huyo ameyalaumu mataifa makubwa kwa
kunyamazia mauwaji yanayoendelea hivi sasa Palestina mwisho amesema
matukio yanayotokea hivi sasa katika nchi ya Nigeria ni njama za kutaka
kuizima harakati ya Kiislamu inayosimamiwa na Sheikh Ibrahim Zakyzaky,
ameendelea kwa kusema kikundi cha Boko haramu ni kikundi
kilichotengenezwa kwa ajili ya kupambana na harakati ya kweli iliyopo
katika nchi hiyo kwani siku zote mkweli uondolewa, Sheikh Hemed Jalala
ametoa salamu za pole kwa kiongozi wa harakati ya Kiislamu Sheikh
Ibrahim Zakyzaky kutokana na msiba mkubwa aliyoupata.