Alhamdulillah
siku ya leo tumeimaliza kwa kufanya matembezi ya kupinga ukandamizaji
dhidi ya wanadamu ulimwenguni, matembezi hayo yamefanyika Kigogo jijini
Dar es Salaam, kwa lengo la kuwaunga mkono wanaharakati wa Palestina
ambao wanaipigania ardhi yao, baadhi ya
Wanaharakati wa Kiislamu wenye misimamo thabiti walijitokeza katika
matembezi hayo ya kuwaunga mkono wapambanaji hao wa Palestina kwa mavazi
ya fulana zenye picha za Viongozi wa Moqawama (Hizbollah) na Masjid
Al-Aqsa na wengine walibeba mabango yenye jumbe mbali mbali pamoja na
picha za wahanga wa Palestina cha hajabu na kusikitisha baadhi ya
VOLUNTEER na viongozi wa matembezi hayo walizuia athari za Moqawama kwa
kuhofia kuonekana wanaunga mkono makundi ambayo Marekani na washirika
wake wameyaweka katika orodha ya magaidi ulimwenguni Viongozi hao na
VOLUNTEER wanadai kuonekana katika jamii athari za Moqawama kutaleta
matatizo na picha mbaya katika harakati zetu, sisi kama wanaharakati wa
Kiislamu na VIjana wa Kiislam tumesikitishwa sana kuona baadhi ya
VOLUNTEER wakimsukuma mtu kutoka meza kuu alipokuwa akichukua habari na
wengine kuvuliwa fulana zao kwa kua wamevaa fulana zenye picha za
Maulamaa ambao Mwaamerika anaitakidi kuwa ni magaidi kwa kweli kitendo
cha kumsukuma Kijana na kumzuia kuchukua habari na kuwavua fulana baadhi
yao ni kitendo cha kidhalili na chakishenzi tunasema sisi kama vijana
na wanaharakati tutasimama kidete siku zote katika kusimamia haki na
kunyanyua picha za Maulamaa popote tulipo kwani kufanya hivyo kuna
baraka kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Hii ni sms niliyotumiwa na
Sheikh kuzuia picha za Maulamaa katika matembezi ya Quds: Salam
alaykum, Bwana Ibrahim nakuomba Sana tushirikiane vyema Kwenye matembezi
ya Leo na kuwa picha pekee zitakazo ruhusiwa kuonekana ni Zile za
viongozi wa kidini na Wala si wa kisiasa, tunafanya hivyo si kwa kuogopa
au kutowatambua Bali ni kwa nia ya kuilinda haraka Yetu. Shukran sheikh
Ghawth. Hapo kamaanisha Picha za Maulamaa ndio za Kisiasa maana tumeona
leo katika matembezi ya Quds zimetawala picha za Mwalimu Nyerere na
Mandera hadi mwisho wa matembezi za Maulamaa zimewekwa kando kwa kuhofia
kuambiwa wanaunga mkono ugaidi kwa kuwa ugaidi unalelewa na Mwamerika.
Astaghafurullah imani yetu ipo wapi enyi ndugu zangu Waislam. Hapa
nakumbuka siku Imam Khomein ( R.A) alipokuwa anafanya harakati za
kuamsha Ummah aliwaona viongozi wa kidini wakirudi nyuma aliwaita na
kuwaambia: Kukaa kimya ni sawa na kuunga mkono dhulma pia alisema:
Tekelezeni wajibu wenu katika dini lolote litakalokuwa na liwe.