Mazishi ya
Chief Kadhi Mubarak yamefanyika leo Madale Saa 10:00 jion, jijini Dar es
Salaam.
Chief Kadhi
Mubarak alifariki ghafla majira ya saa kumi na moja Al fajir nyumbani kwake kwa
Presha, Chief Kadhi alikuwa ni mmoja wa Wanawarisha wa Kiislam (Waandishi wa
Kiislam) na waasisi wa harakati za Kiislam ambao walipigania mafundisho ya
Uislam katika Aridhi ya Tanzania na kufanikiwa kusimamisha maamkizi ya Kiislam
yani “Assalaam Aleykum” na kuifanya salamu ya kawaida katika jamii yetu hadi
sasa na kuleta heshima ya hijabu kwa mwanamke katika jamii ya Kitanzania ambapo
hapo mwanzo vazi la hijabu alikuwa na thamani na maamkizi ya
Kiislam yalikuwa mageni pia walifanikisha kuchapa majalida mbalimbali ya
Kiislam yenye lengo la kuelimisha Ummah wa Kiislam na kusimamisha kituo cha
kutoa elimu ya Msingi hadi Sekondari kwa ajili ya vijana wa Kiislam kilichopewa
jina la Masjid Qubah ambapo ndio kituo Mama na kitovu cha harakati kilichopo
Sinza Mori, jijini Dar es Salaam, baadhi ya waasisi wa harakati hiyo wameonyesha
masikitiko yao kwa kuondokewa na mtu huyo muhimu ambaye ndio alikuwa nguzo
katika kusimamia maendeleo ya harakati hiyo wamesema Chief Kadhi siku zote
alikuwa msitari wa mbele katika mambo yeyote na alikuwa mtendaji mzuri katika
majukumu yake pia walisema Chief Kadhi katika uhai wake alikuwa mara kwa mara hakiimiza
kujitoa katika kusimamia maendeleo ya Ummah bila kusubiri msukumo kutoka kwake,
nijukumu letu sote kufuata njia zake . “Tusome Suratul Fatha kwa ajili ya
Marehemu wote waliotangulia mbele ya haki”