WOSIA WA IMAM KHOMEIN (R.A).

Imam Khomein alikuwa akisema: “Tatizo kubwa la Waislamu ni kuiweka kando Qur’an Tukufu na kuingia chini ya bendera ya wengine.” Pia amesema: “Ushia ambao ni mfumo wa Kimapinduzi na endelezo la Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (S.A.W.W), daima umekuwa ukishambuliwa na Madikteta na Wakoloni, kama walivyofanyiwa Washia wenyewe.”

Mpiga picha wa Chanel ya Al-Manar Tv Shaheed Hamza Hassan meuliwa na magaidi wa Kiwahhab nchini Syria.

Imam Khomein alikuwa akitaja kuuawa Shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni utukufu wa milele, fahari ya mawalii, ufunguo wa saada na ufanisi, na siri ya ushindi. 


Aliitaja hamu ya kupenda Shahada kuwa ni natija ya kumpenda mno Mwenyezi Mungu. "Hakika sisi sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea."