KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.


Hakika kiungo kati ya Uimamu na utume ni Fatima bint Muhammad,
mama wa Maimam maasumina na mbora wa wanawake wote wa
ulimwenguni. Mama yake ni mbora wa wanawake wa kikuraishi,
Khadija binti Khuwaylid bin Asad bin Abdul-Uzza bin Quswayy, na
yeye ndiye mke wa kwanza wa Mtume (s.a.w.w.) na yeye alitokana na
nyumba yenye elimu na sharafu. Hakika kumzaa mtu kama Fatima
Az-Zahrah mkweli, mtakasifu na Maasumu kunatosha kabisa kuwa
utukufu mkubwa kwake.

Tunapenda kuwakaribisha Waislamu wote katika sherehe ya mazazi ya Bibi Fatma Zahrau (a.s) bint wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) itakayofanyika siku ya J.tatu tarehe 21/04/2014, Masjid Al- Ghadiir Kigogo Post jijini Dar es Salaam, kuanzia Saa 4:00 Asubuhi hadi Saa 8:30 Mchana. Fikisha hujumbe kwa wengine.

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika bint yangu amepewa jina la Fatma kwa sababu Mwenyezi Mungu amemtenga mbali na moto yeye na yule atakayempenda.” Rejea: Uyunu Akhbar-Ridha, Juz. 2 Uk. 46. Maanil-Akhbar, Uk. 64. Ilalus- Sharaiu, Uk. 178.