Maandamano ya amani kwa ajili ya kukumbuka kifo cha Mtume (s.a.w.w), yaliyofanyika leo Masjid Al-Ghadiir, Kigogo Post, jijini Dar es Salaam. Mtukufu Mtume Muhammad amefariki tarehe 28 Swafar siku ya Jumatatu mwaka wa kumi Hijria. Familia ya Mtukufu Mtume ilikusanyika kwa ajili ya mipango ya maziko. Umar bin Khattab baada ya kuona familia ya Mtume (s.a.w.w) imekusanyika alichukua Upanga akawa akizunguka huku na kule katika eneo la Misikiti na nyumba ya Mtume (s.a.w.w). Umar bin Khattab kwa sauti yake ya juu akawa anaonya: "Wanafiki wanasema Mtume amekufa, na hakika Mtume hakufa, atakaesema Mtume amekufa nitakata shingo yake." Mpaka alipofika Abubakr Bin Ubu Quhafa akitokea kijijini kwake Sunhi kwa mkewe, akaingia ndani alikolazwa Mtume (s.a.w.w). Alipotoka akasoma Aya:
"Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume aliyepitiwa na Mitume kabla yake. Basi je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu? Na atakaerudi nyuma kwa visigino vyake hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru." 3:144.
Umar akasema:
"Wallahi, kana kwamba watu hawajui kuwa Aya hii ilishuka kwa Mtume."
Kisha Abubakr na Umar wakaondoka kwenda kwenye ukumbi wa Bani Saidah kwa ajili ya Uchaguzi.
Rejea: Tarekh Ibn Athir J.2 Uk. 219, Tarekhut Tabari J.3 Uk. 67-69