Wanaharakati wa Bujumbura, Burundi, wakiwa katika majonzi ya kuondokewa na Kiongozi wa Ummah Mtukufu wa daraja Mtume Muhamma (s.a.w.w). Pindi Mtume alipozidiwa na maumivu hali ambayo ilitokea siku tatu kabla ya kufariki kwake, aliwataka Masahaba wamletee karatasi na wino ili hawaandikie maandiko ambayo kamwe hawatapotea baada yake, Umar bin Al-Khattab akasema: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu anaweweseka, kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu."
Rejea: Sahihi Bukhar, Babu Maradhin-Nabii Wawafatih Juz. 5 Uk. 138.
Haya yote yamefichwa kwa Waislam yasitambuliwe jiulizeni kwa nini Maulid ya Mtume (s.a.w.w), yanafanywa kila kona na kila nyanja na kwa nini siku ya Kifo chake hakuna anayeshughulika nayo zaidi ya Mashia peke yao. Je, Mtume huyo wanayemfanyia Maulid yu hai mpaka leo.?