WAZAYUNI WAHOFIA NGUVU ZA KIJESHI ZA HIZBULLAH.


Viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameeleza kuwa, nguvu za kijeshi za Harakatai ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon zimeongezeka maradufu katika miaka ya hivi karibuni. Yakov Amidror Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Waziri Mkuu wa Israel amesema kuwa, majeshi ya utawala wa Israel yako tayari kukabiliana na vita, lakini akaonya kwamba Hizbullah inaweza kulitingisha jeshi la Israel kwa kutumia udhaifu ulioko kwenye baadhi ya vitengo vya jeshi hilo. Meja Peter Lerner Msemaji wa Jeshi la Israel amesema kuwa, hakuna shaka kuwa vita vijavyo na Hizbullah vitakuwa vikali kuliko vilivyotangulia, kwani makombora ya Hizbullah yana uwezo wa kupiga sehemu yoyote ile ya Israel. Inafaa kuashiria hapa kuwa, wapiganaji wa Hizbullah walifanikiwa kuliondoa kwa madhila jeshi la Israel eneo la kusini mwa Lebanon baada ya kulikalia kwa mabavu kwa zaidi ya miaka 22. Hali kadhalika katika vita vya siku 33, majeshi ya Israel yalikumbana na kipigo kikubwa kutoka kwa wapiganaji wa Hizbullah. Chanzo cha habari http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/36739-wazayuni-wahofia-nguvu-za-kijeshi-za-hizbullah