Hivi
karibuni tulibahatika kushiriki katika sherehe ya harusi, katika
Sherehe hiyo nilipata bahati ya kukutana na Mtunzi wa Mashairi ya
Masahibu ya Karbala, bwana Juma Magambilwa (Juma Shia), amesema sisi
kama wafuasi wa Ahlu-Bayt (a.s) tunawajibu
wa kushirikiana na wafuasi wa Madhihabu ya Sunni katika mambo
mbalimbali, kwani kufanya hivyo kutapelekea kuleta umoja baina yetu kama
Waislamu pia ameongezea kwa kusema maadui wa Uislamu wanapenda kuona
kila wakati Waislamu hawakai sehemu moja na kupanga mambo yao kama
Waislamu na kujiletea maendeleo, amemalizia kwa kuwataka viongozi wa
dini kuto jikweza kutokana na nafasi walizokuwa nazo kwani bado
wanawajibu wa kuwatumikia Wananchi, ameyasema hayo katika Sherehe ya
harusi iliyofanyika Manzese,jijini Dar es Salaam.