Aliyekuwa katibu wa Bakwata ngazi ya Wilaya ya
Kahama hatimae amevuliwa Ukatibu huo baada ya kutangaza rasmi kuwa yeye
ni mfuasi wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah, haya ni matunda ya
mdahalo ulofanyika mjini hapo wiki iliyopita, kwa kweli
Sheikh Masoud ameonyesha Ushujaa mkubwa sana sisi kama wafuasi wa
Madhhebu ya Ahlul-Bayt (a.s) atunabudi kumpokea kwa mikono miwili Sheikh
Masoud pia tumepata funzo kubwa kwa kufukuzwa kwake katika sehemu yake
ya kazi kutokana na kutamka kuwa yeye ni mfuasi wa Madhehebu ya Shia
Ithna Ashariyyah, siku zote sisi tulikuwa tunajua adui yetu ni mmoja tu
WAHHAB (ANSWARU SUNNA) ambaye tunampiga vita karibu Waislamu wote
ulimwenguni anayetumiwa na maadui wa Uislamu kuwagawa Waislamu na kutoa
roho za watu bila ya hatiya yeyote kwa madai ya Jihadi, leo imekuwa
hajabu kuona mambo haya yanatokea kwa jamaa zetu wa karibu, Shia anakosa
gani aliyakuwa anatamka Shahada anafanya ibada ya Hijjah anafuata yale
yote yaliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) na yale yaliyokatazwa
kufanywa ujikataza nayo kuyafanya. Siku zote mti wenye matunda ndio
unaopigwa mawe.
"WAISLAMU WAPI TUNAELEKEA?"
"WAISLAMU WAPI TUNAELEKEA?"