Mnamo mwezi Aprili mwaka huu baadhi ya wanachuoni wa chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar mijini Cairo, nchini Misri, waliitisha Kongamano chini ya anuani ya “Uwahhabi” (Answaru Sunna) hatari kwa Uislamu na Dunia”. Mkutano huo ulibaini kuwa imani za Kiwahhabi zinaimiza vurugu, chuki, hasama, ugaidi na kujitenga na hivyo kuharibu jina na maana ya harakati za Kiisalamu.
Wanazuoni wa Kiislamu wanasema fikra na imani za Kiwahhabi zimejengeka katika msingi wa kuwakufurisha Waislamu wasiokubaliana na mitazamo yao katika masuala yote ya imani. Mbele ya Mawahhabi, Waislamu wa Madhehebu mengine yote kama vile Mashia, Maibadhi, Masunni wa Kishafi, Hanmbali, Maliki, Mahanafi na wengine wote ni makafiri. Fikra kama hizi uzalisha matendo ya kigaidi ni hatari na tishio kwa usalama wan chi zote wanamoishi Waislamu. Hapa Tanzania Mawahhabi wamekuwa chanzo cha vurugu zote zinazotokea katika Misikiti. Mawahhabi ambao wao wenye wanajiita Answaru Sunna kwa kufuata imani yao kuwa wasioamini wanavyoamini wao ni Makafiri, wameanzisha Operesheni ya kuteka Misikiti kwa imani kuwa kufanya hivyo ni Jihadi ya kuwaondoa Makafiri na washirikina katika kuongoza Misikiti.
Katika zoezi hilo wamefanikiwa kuteka Misikiti kadhaa kote nchini na kuikalia huku wadhamini na waasisi wa Misikiti hiyo wakitupwa mikononi mwa vyombo vya dola pindi wanapotaka Serikali kuwasaidia kuirejesha Misikiti yao. Katika hali isiyokuwa ya kawaida kundi la Mawahhabi limefaulu kuendelea kuishikilia Misikiti kwa kutumia mabavu hata pale Mahakama inapotoa amri vyombo vya Dola vinavyohusikia vinaipuuza amri halali ya Mahakama kwa maslahi ya kikundi hiki.
Miradi inayoanzishwa katika Misikiti waliyoiteka, michango ya kila Ijumaa, fedha zinazokusanywa kutoka kwa wafadhili na zile zinazopatikana kila mwisho wa maandamano nisehemu ya mapato yanayokiimarisha kikundi hiki kwa kuwapa uwezo wa kutoa rushwa kwa maafisa wa Serikali wasiokuwa waaminifu ili kuepuka mkono wa sheria za nchi.
Wanazuoni hao wamesema kuwa fedha za Saudi Arabia na uungaji mkono wa Marekani ndio chanzo cha kuenea Uwahhabi duniani. Wameongeza kuwa wakuu wa Riyadh na Washington wanashirikiana kwa Karibu katika kutumia Uwahhabi kwa Marengo yao binafsi. Wanazuoni hao wa Al-Azhar wamesema kuna udharura wa kubuniwa njia muafaka za Kiislamu za kukabiliana na ugaidi.
Mwndelezo wa machafuko na umwagaji damu nchini Iraq umezua maswali mengi kuhusu wahusika halisi na wale walioko nyuma ya pazia la matukio hayo ya umwagaji damu. Hata hivyo ni vyema kuashiria hapa kwamba, makundi ya kigaidi yanayokufurisha Waislamu, yanayofanya kazi kama vikaragosi wa baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo, Saudi Arabia, Qatar, utawala haramu wa Israeli na Marekani. Waledi wa mambo wanaamini kuwa, ni fikra finyu kudhani kwamba makundi ya kigaidi yaliyoko ndani ya ardhi ya Iraq na kwengineko duniani, ndio pekee yanayohusika na njama ya kuvuruga amani na usalama wanchi hizo. Soma Gazeti la MIZANI kila Ijumaa