Assalaam Aleykum, Tunapenda kuwakaribisha Waislam wote katika Matembezi ya Amani ya kukumbuka kifo cha Mtukufu wa daraja Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w), Matembezi hayo yatafanyika tarehe 2/01/2014 siku ya Alhamisi Saa 3:00 Asubuhi kuanzia Shule ya Msingi ya Lutihinda, iliyopo Kigogo mpaka Masjid Al-Ghadiir Kigogo Post, jijini Dar es Salaam. Fikisha ujumbe kwa wengine Insh'allah, japokuwa tukio la kufishwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) mbele ya jamii ni jambo geni sana, kana kwamba katika historia ya ulimwengu tukio hili halikutokea. Ingawa tukio la kuzaliwa kwa Mtume Muhammad limepokelewa kwa nafasi kubwa isiyo kifani. Kwa hiyo, unaweza kuona hafla mbalimbali za kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) zikifanywa Misikitini, Madrasani, Majumbani, na katika Mazawia mbalimbali. Hili ni jambo jema sana, swali liliyopo hapa ni, je, huyu afanyiwae haya yu hai mpaka sasa? Au amekwisha kufa? Ni kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) amekwisha kufa. Sasa, tarehe ya wafat wa Mtume, Waislamu wanaichukuliaje. Inafaa ikumbukwe tarehe hiyo ya wafat tarehe ambayo Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndiyo alioaga dunia, au haifai kuikumbuka?! Ilikuwaje! Maulamaa wa Kiislamu na Masheikh wa Twariqa katika tarehe zao za wafat hukumbukwa kwa visomo mbalimbali. Hili ni jambo jema, isipokuwa tarehe ya wafat wa Mtume Muhammad!!!
TANGAZO.