MANENO KUTOKA KATIKA AYA ZA QUR'AN TUKUFU.


Na ni nani dhalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo na hali anaitwa kwenye Uislamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu. 
(Qur'an: 61:7)

Wanataka kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ingawa makafiri watachukia. 
(Qur'an:61:8)

Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu hayo ni bora kwenu ikiwa mnajua. 
 (Qur'an: 61:11)

Enyi mlioamini! kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu kama alivyosema Issa bin Mariam kuwaambia wafuasi (wake): Ni nani wasaidizi wangu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi taifa moja la watu wa Israeli walioamini, na taifa jingine wakakufuru, ndipo tukawasaidia wale walioamini juu ya maadui zao na wakawa wenye kushinda. 
(Qur'an: 61:14)