Hakika sisi sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na
kwake tutarejea. Sheikh Ibrahim Mlosi amefariki usiku wa kuamkia leo kwa
Ugonjwa wa Figo, mazishi yatafanyika Saa Kumi jioni nyumbani kwake
Mbagala Nzasa, kwa mawasiliano zaidi unaweza kupiga simu namba
0786750004
Sheikh
Mkuu wa Tanzania Ithna Ashariyyah, Abdallah Seif akiongoza swala ya
Jeneza katika mazishi ya Sheikh Ibrahim Mlosi, yaliyofanyika leo Mbagala
Nzasa, jijini Dar es Salaam. Marehemu alikuwa ni mtu wa pekee katika
jamii alijitoa Muhanga maisha yake kwa ajili ya kusimamia Madhihebu ya
Ahlul-Bayt(a.s) yasonge mbele katika aridhi ya Tanzania, nani kama
Ibrahim Mlosi? Kuondokewa na mtu huyu muhimu kwetu sisi tumepata pigo
kubwa sana kama Wanaharakati na wapenda haki, tunapenda kutoa wito kwa
vijana wengine wafuate nyayo za Sheikh Ibrahim alikubali kuicha dunia na
kuifuata Akhera.
Tunapenda
kuwakaribisha katika kisomo cha Dua kwa ajili ya ndugu yetu, kijana
mwenzetu, Mwanaharakati mpenda haki Sheikh Ibrahim Mlosi
kitakachofanyika kesho Masjid Al-Ghadiir Kigogo Post, jijini Dar es
Salaam, baada ya Swala ya Magharib. Mjulishe mwengine Insh'allah.