‘IRAN IMO MBIONI KUTATUA KADHIA YA NYUKLIA KISHERIA’


Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran imo mbioni kutatua kadhia ya nyuklia katika fremu ya sheria. Dakta Hassan Rouhani amesema hayo katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Dmitry Rogozin, Naibu Waziri Mkuu wa Russia na kusisitiza kwamba, Iran itaendeleza juhudi zake zenye lengo la kuipatia ufumbuzi kadhia yake ya nyuklia katika fremu ya sheria na mikataba ya kimataifa. Rais wa Iran amesisitiza kwamba, Iran haina mpango wa kuzalisha silaha za mauaji ya umati. Rais Rouhani ameashiria katika mazungumzo hayo juu ya maslahi ya pamoja ya Iran na Russia katika Mashariki ya Kati  na katika uga wa kimataifa na kubainisha kwamba, Tehran na Moscow zina uhusiano wa kirafiki na mkongwe na kwamba, kuna haja ya kustawisha zaidi uhusiano wa pande mbili. Kwa upande wake Dmitry Rogozin, Naibu Waziri Mkuu wa Russia ameelezea hamu na shauku kubwa ya Moscow ya kustawisha uhusiano wake na Tehran.Chanzo cha habari http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/36265-‘iran-imo-mbioni-katika-kutatua-kadhia-ya-nyuklia-kisheria’