Harakati ya Mapambano Kiislamu ya Hizbullah ya
Lebanon imetahadharisha kuhusiana na harakati za makundi ya ukufurishaji ya
kigaidi huko nchini Lebanon. Tahadhari hiyo imetolewa na Sheikh Nabil Kaouk,
Naibu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Hizbullah ambaye amesisitiza kwamba,
kuna haja ya kuchukuliwa hatua madhubuti za kukabiliana na makundi ya
ukufurishaji ambayo yana mfungamano na utawala haramu wa Israe. Sheikh Nabil
Kaouk amesema kuwa, mlipuko wa Jumanne iliyopita mjini Beirut mkabala na
ubalozi wa Iran ni njama za Wazayuni na kwamba, makundi ya ukufurishaji
yanayoendesha harakati zao nchini Lebanon ndio yaliyotekeleza njama hiyo.
Ameongeza kuwa, Hizbullah mara chungu nzima imetahadharisha kuhusiana na hatari
ya harakati za magaidi wa al-Qaeda na matakfir nchini Lebanon na kwamba,
mlipuko wa hivi karibuni umethibitisha madai ya muqawama. Aidha Naibu wa Baraza
la Utendaji la Hizbullah amebainisha kwamba, lengo la milipuko kama hiyo ni
kudhamini maslahi ya utawala haramu wa Israe.