Bissimillah Taa'allah
Mwenyezi Mungu anasema kumwambia Mtume wake (s.a.w.w) kuwa: “Wala
usivikodolee macho yako tulivyowastaresha watu wengi miongoni mwao, ni mapambo
ya maisha ya dunia, ili tuwajaribu kwa hayo, na riziki ya Mola wako ni bora mno
na iendeleayo.” Taha: 131
Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa mkweli katika kuicha
dunia na mapambo yake. Aliicha dunia mpaka ikapokewa kutoka kwa Abu Ummah
kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Mola wangu alinitunukia
akataka aifanye Makka yote iwe dhahabu kwa ajili yangu, nikasema: Hapana Mola
wangu! Lakini napenda niwe nashiba siku moja na kushinda na njaa siku nyingine………..Kwani
nitapokuwa na njaa nitakunyenyekea na kukukumbuka, na nitakaposhiba
nitakushukuru na kukuhindi.”
Rejea: Sunani Tirmidhiy, Juz. 4 Uk. 1518 na 508, hadithi ya
2377 na 2360.
Akalala juu ya changarawe na alipoamka zilikuwa zimeathiri
ubavu wake. Akaambiwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tungekuweka kizuwizi.”
Akajibu: “Mimi nina nini na hii dunia, kwani mimi si chochote ndani ya dunia
hii isipokuwa ni kama msafiri aliyejipumzisha chini ya mti wa kivuli na baada
ya mapumziko ataondoka na kuuacha ule mti.”
Ibn Abbas anasema: “Mtume (s.a.w.w) alikuwa akilala njaa
siku zenye kufuatana, huku familia yake ikiwa haipati chakula cha usiku. Mara nyingi
mkate wao ulikuwa ni mkate wa shairi.”
Swali: Je, mimi
na wewe leo hii tumeipa mgongo dunia katika harakati zetu?