UTAWALA HARAMU WA ISRAEL WAENDELEA KUUZA SILAHA NCHINI BURMA.


Nchi ya Israel ipo katika tuhuma nzito kutoka ka mashirika ya kutetea haki za binaadamu, kwa kitendo chake cha kuendelea kuizuia silaha jeshi la nchi ya Burma mbali na mauaji dhidi ya jamii ya Waislam walio wachache katika nchi hiyo.
Uchunguzi wa mashirika ya kupigania haki za binadamu umebaini kuwa zaidi ya vifaru vya kijeshi 100, pamoja na merikebu na silaha nyingine ndogondogo, zimeuzwa kwa serikali ya Burma na makampuni ya kiisareli.

Kampuni moja la kiislaeli liitwalo TAR Ideal Concepts, ambalo limekuwa likitoa mafunzo ya kwa vikosi maalumu katika jimbo la kaskazini la Rakhine. Jimbo hilo ndilo ambalo mauaji yanafanyika llimeweka picha katika mtandao ukiwaonesha wafanyakazi wake wakitoa mafunzo ya kivita na namna ya kushikilia silaha.
Nchi za ulaya EU pamoja na Marekani ziliiwekea vikwazo nchi ya Burma vya kuiuzia silaha vikwazo ambavyo bado vinafanya kazi.
Ofer Neiman mwanaharakati wa haki za binaadamu amenukuliwa na shirika la habari la Middle East Eye akisema “Serikali imekuwa ikiiuzia silaha jeshi la kidikteta la Burma kwa miaka mingi sasa”.
Picha za watoto wakiwa wamekatwa vichwa na vijiji kuteketea kwa moto kulikofanywa na jeshi la Burma zimeenea duniani kote.

chanzo cha habari: www.Independent.co.uk