BHRN: SIO WAISLAMU WA RAKHINE TU WANAOUAWA MYANMAR.
Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Myanmar limetoa ripoti iliyofichua kuwa Waislamu katika maeneo yote ya nchi hiyo wanauawa na kuhujumiwa na wanajeshi wa nchi hiyo na sio wa kabila la Rohingya tu katika mkoa wa Rakhine.
Ripoti iliyotolewa jana Jumanne na Burma Human Rights Network imesema kuwa, serikali inawaunga mkono wanajeshi na mabudha wenye misimamo mikali kuwashambulia Waislamu katika kila pembe ya nchi hiyo ya mashariki mwa bara Asia.
Ripoti hiyo imesema kuwa, mbali na Waislamu wa Myanmar kunyimwa huduma za msingi kama matibabu wanapokwenda hospitalini, lakini pia serikali imekataa katakata kuwapa vitambulisho vya taifa.
Ripoti ya Burma Human Rights Network imebainisha kuwa, Waislamu katika miji na vijiji 46 nchini Myanmar wanapitia kila aina ya jinai kutoka kwa askari wa jeshi la nchi hiyo wakishirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali.
Tangu tarehe 25 Agosti mwaka huu, jeshi la Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali limekuwa likiwashambulia Waislamu wa jimbo la Rakhine, ambapo zaidi ya 400 miongoni mwao wamekwishauawa, huku wengine zaidi ya laki 1 na 25 elfu wakikimbilia Bagladesh.
Mauaji na jinai hizi zinafanyika mkabala wa kimya cha taasisi husika za kimataifa kama vile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.KUENDELEA KUULIWA WAISLAMU WA ROHINGYA NCHINI MYANMAR.
Wawakilishi wa bunge la Myanmar wametaka kujengwa vijiji zaidi vya kikabila kwa lengo la kuwakandamiza Waislamu wa jamii ya Rohingya ikiwa ni katika kuendelea kuangamizwa kizazi cha Waislamu hao huko Myanmar khususan katika mkoa wa Rakhine.
Aghalabu ya Waislamu wa Rohingya wanaishi katika mkoa huo unaopatikana magharibi mwa Myanmar. Pamoja na kuwepo mkakati wa kuwafukuza Waslamu wa Rohingya katika mkoa wa Rakhine, wabunge wa Myanmar wanakiri kuwa tangu maelfu ya miaka nyuma, eneo hilo limekuwa makazi asilia ya Waislamu wa Rohingya tangu enzi za mababu likijulikana kwa jina la Aragan, na vile vile lilikuwa na utawala wa kifalme kwa muda wa miaka mia tatu. Hata hivyo mashinikizo dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya yalianza rasmi katika muongo wa sitini miladia baada ya kuingia madarakani wanajeshi nchini humo; na kisha mashinikizo hayo kuendelezwa kufutia vitisho na uchochezi wa watawala wa Kibudha wenye misimamo mikali kama Ashin Wirathu. Kwa kadiri kwamba kuanzia mwaka 2012 Waislamu wa Rohingya zaidi ya elfu moja waliuawa na wengine zaidi ya laki moja kulazimishwa kuwa wakimbizi katika nchi jirani kutokana na ukandamizaji na mauaji ya umwagaji damu yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo ya kufurutu ada.

Utekelezaji wa mauaji au maangamizi ya kizazi ya Waislamu wa kabila la Rohingya umebadilika na viongozi wa serikali na wale wa kieneo wameazimia kuasisi vijiji vya kikabila ili kuwanyang'anya ardhi jamii hiyo kwa kuzingatia radiamali inayotolewa na jamii ya kimataifa kwa mauaji ya kizazi huko Myanmar na pia kuwahusu viongozi wa nchi hiyo khususan Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala cha National League for Democracy (NLD) ambaye pia ni mshauri wa ngazi ya juu wa serikali ya nchi hiyo. Siasa hizo zinafuatliliwa kwa jadi na kupewa kipaumbele cha awali na wabunge wa Myanmar ambao wengi ni kutoka chama cha National League for Democracy chini ya uongozi wa Bi Suu Kyi. Jenerali Than Htut Naibu Waziri Anayehusika na Masuala ya Mipaka wa Myanmar amesema kuwa vijiji 36 vya kikabila vimejengwa katika maeneo tofauti mkoani Rakhine na kwamba serikali ina mpango wa kuyahamisha makabila mbalimbali kutoka katika eneo la Yangon na kuyapeleka katika maeneo hayo lengo likiwa ni kuvuruga muundo wa kijamii wa mkoa wa Rakhine na hivyo kuwadhihirisha Waislamu wa Rohingya kuwa ni jamii ya waliowachache. Kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2016 hadi Februari mwaka huu maeneo ya Buthidaung na Mandau katika mkoa huo yamekumbwa na mashambulizi ya umwagaji damu ya Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu wa Rohingya.

Kwa kuzingatia nafasi nzuri ya kijiografia ya mkoa wa Rakhine kwa upande wa hali ya hewa na ardhi ya kilimo na vile vile shughuli za kibishara, ni karibu miongo sita sasa ambapo Mabudha wenye misimamo mikali wameanzisha jitihada kubwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za kiuongozi na kijeshi ili kupora na kumiliki ardhi, vituo vya kibiashara na kuwadhibiti Waislamu wa Rohingya; ambapo lengo lao kuu ni kuwafukuza katika makazi na nyumba zao kwa kutekeleza mauaji ya kizazi dhidi ya jamii hiyo. Pamoja na hayo yote, kusimama kidete na kuendesha muqawama Waislamu wa kabila la Rohingya mkabala na mashinikizo na ukandamizaji wa Mabudha wenye misimamo ya kuchupa mipaka huko Myanmar kumekwamisha kutekelezwa siasa za kuangamiza kizazi dhidi ya jamii hiyo iliyodhulumika; na hilo ndilo limewafanya watawala wa nchi hiyo wakimbilie kuasisi vijiji vya kikabila ambavyo hakuna matarajio kwamba vitaweza kufanikisha mkakati wao wa kuwafukuza Waislamu wa Rohingya katika ardhi zao asilia. http://parstoday.com/…/world-i30216-kuendelea_kuuliwa_waisl…