Kwa
mujibu wa mwandishi wa IQNA, nchini Tanzania kumefanyika halfa kubwa za Taasua
(Tisa Muharram) na Ashura (10 Muharram) katika kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu
wa Mtume Mtukufu SAW, Imam Hussein AS na wafuasi wake 72 watiifu katika jangwa
la Karbala. Maelfu ya Waislamu walishiriki katika maombolezo hayo.
Moja ya
hafla hizo ni ile iliyofanyika katika Madrassah ya Al Hudaa ambapo mwambata wa
utamaduni wa Iran nchini Tanzania Ali Baqeri alihutubu na kusema Imam Hussein
AS alikuwa shujaa ambaye hadi lahadha ya mwisho alipipamana kwa ajili ya
Tauhidi na kumuabudu Mwenyezi Mungu. Aidha mjini Dar es Salaam kulifanyia
matembezi (masir) katika siku ya Taasua ambayo yaliwashirikisha watu wa
matabaka mbali mbali katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi hadi katika Msikiti
wa Jamia ywa Khoja Shia Ithnaashari. Viongozi wa Kishia na Kisunni walishiriki
katika mjumuiko huo akiwemo Shehe Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Mussa Salim Al
Hadi.
Akihutubu
katika kikao hicho, Sheikh Hadi alisema: 'Ashura ni kati ya Siku za Allah na ni
siku ya huzunu kwa Waislamu na Uislamu. Ashura haina madhehebu maalumu na ni ya
Waislamu wote." Aidha aliashiria nafasi maalumu ya Bibi Fatima Zahra SA na
Imam Ali AS mbele ya Mtume SAW na kusema: "Hussein AS alikuwa mjukuu wa
Mtume SAW na aliuawa shahidi kidhalimu huko Karbala." Sheikh al Hadi
amekumbusha kuwa Mtume SAW alisema: "Mwenye kumpenda Al Hassan na Al
Hussein amenipenda na mwenye kuwachukia amenichukia."
http://iqna.ir/sw/news/3470614/kumbukumbu-ya-ashura-ni-katika-nembo-za-allah