Maelfu ya watu wa Iran leo wameshiriki katika mazishi ya Ayatullah Abbas
Va’ez Tabasi, Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha AS, katika mji
wa Mash'had kaskazini mashariki mwa nchi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliongoza mazishi hayo na kusalisha Swala ya Maiti ya Ayatullah Va’ez Tabasi.
Rais Hassan Rouhani na Spika wa Bunge Ali Larijani walikuwa miongoni mwa maafisa wa ngazi za juu Wairani waliohudhuria mazishi hayo katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Iran.
Ayatullah Tabasi aliaga dunia Ijumaa ya jana akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kulazwa hospitalini kwa muda wa wiki moja. Ayatullah Khamenei, Rais Rouhani pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu nchini walituma salamu za rambirambi na kumuenzi mwanazuoni huyo wa kidini aliyejitolea umri wake wote kuuhudumia Uislamu na Waislamu.
Ayatullah Tabasi alihudumu kama Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha AS na taasisi ya waqfu inayosimamia Haram hiyo tokea baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979. Aliteuliwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini MA kuchukua nafasi hiyo na alikuwa pia mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu Wa Iran, mwanachama wa Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu na mwakilishi wa Faqihi Mtawala katika eneo la Khurassan.