Taasisi ya Bilal Muslim Mission ya Tanzania kwa kushirikiana na watu
wote watakao uhuru na haki, wanadhihirisha mshituko wao kwa hukumu ya
kifo iliyotolewa kwa Sheikh Nimr Baqir Al-Nimr kutokana na yeye kudai
kutokuwepo kwa uadilifu na haki sawa kwa raia wote wa nchini Saudia
Arabia.
Tunaomba ushirikiano na mshikamano kutoka kwa watu wote wapendao amani katika dunia hii kuzitaka mamlaka za Saudia Arabia kufuta kabisa hukumu hiyo ya kifo dhidi ya Sheikh Al Nimr. Kwamba Serikali imuache huru kwa kuzingatia vipimo na misingi ya Demokrasia iliyotangazwa na kuhifadhiwa kwa heshima kubwa ndani ya hata/Mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za binadamu.
Hakupaswi kuwa na taifa lolote katika familia ya mataifa ambalo litajipa mamlaka ya kisiasa ambayo ni nje ya Jamhuri ya Demokrasia (Dola inayofuata misingi ya Demokrasia). Jambo lengine lolote zaidi ya hilo ni ukiukwaji wa hadhi na heshima ya binadamu.
Hakuna mtu yeyote atakayelazimika kupokonywa uhai wake kwa ajili ya kusimama ili kupigania na kutetea haki za binadamu kwa kiwango ambacho kinahakikisha kuwepo kwa Demokrasia, Uhuru wa kujitawala na Uadilifu wa kijamii pamoja na Usawa.
Jamii ya binadamu lazima isimame kama familia moja kusimama kidete kudai haki zake za heshima, hadhi ya kibinadamu na Utu, haki ya uhuru wa kujieleza, haki ya Demokrasia, Uhuru wa kujiamulia mambo na kujitawala au kujiongoza.
KIFO CHA MTU MMOJA WA AINA HIYO, MWENYE KUPOKONYWA MAISHA YAKE KWA KUPIGANIA HAKI, NI DHIMA KWA BINADAMU WOTE.