RAFSANJANI: ISRAEL ITAFUTWA KATIKA RAMANI YA DUNIA.

Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu nchini Iran amesema kuwa suala la kufutwa utawala bandia wa Israel ni mwenendo ambao hauwezi kuepikwa.
Ayatullah Hashemi Rafsanjani amesema kuwa kuwepo kwa utawala bandia wa Israel ni suala la muda tu na kwamba hatimaye utawala huo utafutwa.
Kuhusu mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea huko Vienna nchini Austria kati ya Iran na kundi la 5+1, Ayatullah Rafsanjani amesema kuwa Israel imekuwa ikifanya njama za kutaka kukwamisha mazungumzo hayo na kwamba baadhi ya nchi za Kiarabu zinafuata sera hizo za Israel.
Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Suadi Arabia dhidi ya watu wa Yemen ni makosa ya kistratijia ya watawala wa Aal Saud. Vilevile amezungumzia umuhimu wa Siku ya Kimataifa ya Quds inayoadhimishwa na Waislamu katika Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuonesha uungaji mkono wao kwa Wapalestina wanaoendelea kuuawa na maghasibu wa Israel na akasema: Hatua ya Imam Khomeini ya kuitangaza siku hiyo imekuwa na taathira kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Chanzo ni:http://kiswahili.irib.ir/…/49987-rafsanjani-israel-itafutwa…