TANGAZO

Jukumu letu sote kusimama imara kuonesha ulimwengu misimamo yetu juu ya upingaji unyanyasaji na ukatili unaofanyika dhidi ya wanadamu ulimwenguni, jamii yeyote inapoona unyama na ukatili unatendeka na kukaa kimya jamii hiyo aina tofauti na jamii maiti na jamii hiyo siku zote itakuwa ikiomboleza misiba na ukandamizaji. Leo hii unyama huu unafanyika kwa jamii ya WAPALESTINA tujiulize je, kesho kwa nani unyama huu utaelekezwa? Ni vyema kusema na kupaza sauti kukemea haya kulikokufumba macho yetu. Daima tusikubali ukandamizaji kwetu na kwa wengine.
Vitendo vinavyofanyika leo hii katika ardhi ya PALESTINA ni vitendo vya kinyama kwa kweli kwa mwenye moyo wa imani na kujali utu wa mwanadamu kamwe hawezi kuvumilia, hakuna jamii ambayo inapendezwa kuishi maisha ya mashaka na dhiki lakini watu WAPALESTINA wao siku zote wamekuwa katika hali ya mashaka na vifo kila kukicha.
"KUKEMEA VITENDO VYA UNYANYASAJI DHIDI YA WAPALESTINA NI WAJIBU WETU."