MANENO YA HEKIMA YA IMAM KHOMEIN (R.A).

Imam Khomein (r.a) amesema kwamba: "Askari wa kujitolea" ni jeshi la watu wanyoofu wa Allah na ni vipenzi wa Allah. Dini ya "Askari wa kujitolea" sio ile ya biashara na uchuuzi. "Askari wa kujitolea" sio mtu ambaye anakuja katika uwanja wa mapambano kwa ajili ya HURULAIN (WAnawake wa Peponi); anakuja katika uwanja wa mapambano kwa ajili ya Mapenzi ya Allah. "Askari wa kujitolea" anatambua kila kitu (maana yake matokeo ya harakati zake) na yuko katika kila uwanja. Imam Khomein (r.a). anasema ni muhimu kwa "Askari wa kujitolea" kuwepo katika viwanja mbalimbali. Moja ni katika kambi ya maadui wa kiulimwengu ambayo ni Uzayuni na Marekani ambao watakabiliana na "Askari wa kujitolea". Kambi nyingine ni ile ya propanganda za uenezaji wa propanganda ambayo pia itapambana na "Askari wa kujitolea". Mtu ambaye ni "Askari wa kujitolea" ni mtu ambaye anafahamu na amejiandaa. Anafahamu kuhusu dini yake, kuhusu wajibu wake, kuhusu kazi yake, anafahamu kuhusu maadui zake na mbinu za maadui. Kama umevaa Skafu ya "Askari wa kujitolea" na kujaribu kujionesha mwenyewe kama "Askari wa kujitolea" basi elewa ukweli huu kwamba Allah amekuteua kwa ajili ya jukumu hili na sasa lazima uwe mzoefu na kutambua kuhusu viwanja vyote vile ambavyo kwavyo unahitajika kuwepo. Lazima uwe na utambuzi kuhusu dini yako na utambuzi kuhusu mapinduzi. "Askari wa kujitolea" ni mtu ambaye ana ghera kwa ajili ya Mapinduzi.