KARBALA.

Kwa jina la Allah! Kama Waislam wangeilewa Karbara leo wasingekuwa wana maisha haya ya udhalili kwa sababu Karbala ni njia ya heshima, adabu, utukufu na maadili. Na ni jukumu letu kuwajulisha watu kuhusu njia hii ya heshima. Watawala wetu ambao wametoka kwenye vyuo vikuu vya Marekani hawatambui ni jinsi gani Karbala ni njia ya heshima, hivyo ni jukumu la jumuiya yetu kuwajulisha hata watawala kwamba kama wanataka kutembea kwenye njia ya heshima basi njia hiyo ni Karbala. Ni jukumu la Mimbari hii kuonesha nchi hii na mataifa mengine yote ya ulimwengu kwamba njia ya ukombozi ni Karbala. Ni jukumu la kazi hii ya Maombolezo ya kifo cha Hussein (a.s), ya Nawha, ya visomo na ya kupiga vifua, na kila mtu na kila kitu kinachofanywa kwa jina la Maombolezo ya kifo cha Hussein (a.s) lazima kioneshe ulimwengu njia ya heshima na ukombozi. Lakini ni ngumu kwa sababu njia ya heshima ni njia ya panga na kwa hiyo ni vigumu kutembea katika njia hii. Hii ndio sababu watu wanakimbilia udhalili kwa sababu ni rahisi. Vilevile; gharama ya kulipa katika njia ya heshima ilioneshwa na Karbala, Wakati msafara huu ulipoanza kutoka Madina, Mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) Ummu Salma alimshauri Hussein (a.s) asiende. Yeye (a.s) alijibu kwamba " Allah anakusudia kuniona mimi nikiuawa shahidi." Kisha alimtaka angalau basi asichukue wanawake na watoto pamoja naye. Yeye (a.s) akajibu: "Allah anakusudia kuwaona wanawake hawa wa familia yangu kama mateka waliofungwa kamba na minyororo." Hii ilikuwa ni gharama ambayo ililipwa kwa ajili ya kuwa katika njia ya heshima. 

Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi