AL: KUPAMBANA NA UGAIDI NI KUUTETEA UISLAMU.

Washiriki wa kikao cha dharura cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kilichofanyika mjini Cairo, Misri wamesema kuwa, kupambana na ugaidi ni suala lenye kipaumbele zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu kwa ujumla. Taarifa iliyotolewa mwishoni mwa kikao hicho cha dharura imesema kuwa, kukabiliana na ugaidi ni kupigania Uislamu na kwamba hilo ndilo suala la msingi kwa Waislamu wote duniani. Aidha washiriki wa kikao hicho wameitaka jamii ya kimataifa kuonyesha uungaji mkono wao kwa nchi za Kiarabu na Kiislamu, katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo linalotishia usalama wa dunia. Jumuiya hiyo imesisitizwa kuwa, kukata mizizi ya ugaidi, kunahitajia kwanza ushirikiano wa nchi zote za Kiarabu na kudhaminiwa fedha katika uwanja huo. Aidha washiriki wa kikao hicho wamelaani vikali ugaidi wa hivi karibuni nchini Kuwait, Tunisia na Misri na kuutaja ugaidi kuwa tishio kwa usalama wa eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu kwa ujumla. Hayo yanajiri katika hali ambayo, ni Jumuiya hiyohiyo ya Arab League ndiyo iliyotoa baraka kwa makundi ya kigaidi kama vile Daesh, Jab’hatu Nusra na mengineyo huko Syria kwa ajili ya kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/49824-arab-league-kupambana-na-u…