AL-AZHAR: LIWEPO JESHI LA KIARABU DHIDI YA MAGAIDI.

Kiongozi wa Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri Ahmad al-Tayib, ametaka kuundwe kikosi maalumu cha nchi za Kiarabu kitakachokuwa na jukumu la kukabiliana na makundi ya kigaidi. Ahmad al-Tayib ameyasema hayo katika sherehe za kufunguliwa kongamano la 24 la kimataifa la Baraza Kuu la Mambo ya Kiislamu na kuongeza kuwa, ugaidi unaoendelea ndani ya nchi za Kiarabu, hauwezi kuangamizwa kinyume na majeshi yasiyo ya Kiarabu. Kiongozi wa Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri amesisitiza kwamba, katika kumaliza makundi ya magaidi, Waarabu wanatakiwa kubeba silaha na kuzielekeza kwa makundi hayo. Aidha amesisitiza juu ya udharura wa kuyaunganisha pamoja majeshi hayo ya Kiarabu kwenye jeshi la serikali ya Misri ili kufanikisha kung'oa mizizi ya makundi ya kigaidi. Kabla ya hapo pia Rais Abd Al- Fattah al Sisi wa Misri alitoa pendekezo la kuundwa kikosi cha nchi za Kiarabu kwa ajili ya kukabiliana na ugaidi. Hivi karibuni pia Sheikh Ahmad al-Tayib, alitoa mwito kwa nchi za Kiislamu kufanyia marekebisho mitalaa ya elimu katika taasisi za elimu ili kupunguza wimbi la vijana kujiunga na makundi ya kigaidi duniani. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/47029-al-azhar-kuwepo-jeshi-la-k…